• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Rigathi Gachagua na Moses Kuria wakabana koo kuhusu ‘ndoa’ ya UDA

Rigathi Gachagua na Moses Kuria wakabana koo kuhusu ‘ndoa’ ya UDA

SUALA la ikiwa chama cha UDA, chake Naibu Rais Wiliam Ruto kinafaa kubuni miungano ya kisiasa au la bado linaendelea kuzua majibizano baina ya washirika wake wa karibu.

Hii ni licha ya Dkt Ruto kusema kuwa yuko tayari kushirikiana na vyama vingine, bila kuwashinikiza viongozi wake kuvivunja kama sharti la kujiunga na UDA.

Licha ya hakikisho hilo, wabunge Rigathi Gachagua (Mathira) na Moses Kuria (Gatundu Kusini) walikabiliana vikali wiki hii, kila mmoja akieleza hisia tofauti kuhusu suala hilo.

“Ikiwa unaamini chama chako kina nguvu na ushawishi mkubwa kisiasa, hilo litadhihirika wazi baada ya uchaguzi wa Agosti. Imekuwa kawaida kwa viongozi wa kisiasa kubuni vyama vya kikabila kila wakati wanapoona ama kuhisi ushindani dhidi yao umeongezeka. Hatuna masharti yoyote, ijapokuwa ni wakati viongozi wanaojificha katika vyama vidogo vidogo wajitokeze wazi.” na kieleza nia zao.”

  • Tags

You can share this post!

Mijeledi ya John Michuki ilivyolainisha sekta ya matatu

Raila ‘adandia’ sifa ya Kibaki kukwea Mlima...

T L