• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Tiketi ya ODM yavutia wengi wanaotaka kurithi Ojaamong

Tiketi ya ODM yavutia wengi wanaotaka kurithi Ojaamong

Na LEONARD OWINO ONYANGO

Na KENYA NEWS AGENCY

KINYANG’ANYIRO kikali cha kutaka kumrithi Gavana wa Busia Sospeter Odeke Ojaamong kinatarajiwa huku idadi ya wanasiasa waliojitokeza kung’ang’ania tiketi ya chama cha ODM ikizidi kuongezeka.Wanasiasa watano tayari wametangaza azma ya kuwania kiti hicho kupitia chama cha ODM mwaka ujao.

Wanasiasa hao sasa wanatafuta uungwaji mkono kutoka kwa kiongozi wa ODM Raila Odinga, hata baada ya Bw Ojaamong kutangaza kwamba ataunga mkono naibu wake, Moses Mulomi.“Nimefanya kazi na naibu wangu tangu 2017 na ameonyesha utiifu na uvumilivu wa hali ya juu. Ninatangaza kwamba Bw Mulomi ndiye atakuwa gavana wa pili wa Busia,” akasema.

Wanasiasa wengine ambao wametangaza azma yao ya kuwania ugavana kupitia tiketi ya chama cha ODM ni Seneta wa Busia Amos Wako, Mwakilishi wa Wanawake Florence Mutua, mbunge wa zamani wa Funyula Dkt Paul Otwoma na Dkt Lucas Meso.

Bw Odinga atajipata katika njiapanda kuhusu mwanasiasa atakaye muunga kurithi Bw Ojaamong.Bw John Sakwa Bunyasi ametangaza kuwa atawania wadhifa huo kupitia chama cha ANC na Mhandisi Vincent Sidai atagombea kupitia Ford Kenya.

Ukabila na desturi ya siasa vinatarajiwa kuamua atakayemrithi Bw Ojaamong.’Tulikubaliana kwamba Bw Ojaamong anayetoka jamii ya Wateso awe gavana na naibu wake atoke upande wa Waluhya. Mwaka ujao, Wateso watatoa naibu gavana na Waluhya watatoa gavana,” akasema mbunge wa Matayos Geoffrey Odanga.

Bi Mutua ambaye sasa ni mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Bungeni, amekuwa katika mstari wa mbele katika kuendesha ajenda ya chama cha ODM katika Kaunti ya Busia na eneo la Magharibi.

  • Tags

You can share this post!

Familia 100 zilizopoteza nyumba zao katika kisa cha moto...

Ndege iliyobeba abiria 40 yatua ghafla