• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 5:50 AM
Tumepata ushahidi wa kubatilisha ushindi wa Ruto – Mawakili

Tumepata ushahidi wa kubatilisha ushindi wa Ruto – Mawakili

NA GEORGE MUNENE

MAWAKILI wa mgombea urais wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga wamesema kuwa, wamekusanya ushahidi wa kutosha kuwawezesha kubatilisha ushindi wa Rais Mteule William Ruto katika Mahakama ya Juu.

Mmoja wa mawakili hao, Ndegwa Njiru jana Ijumaa alifichua wako tayari kuthibitisha kuwa kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi wa urais.

“Tumepata ushahidi wa kutosha kuhusu wizi wa kura za urais na tutathibitisha hilo mbele ya majaji saba wa Mahakama ya Juu,” akasema.

Bw Njiru alisema Wakenya wanasubiri kwa hamu kujua kilichotokea wakati wa uchaguzi huo wa Agosti 9 ili wajue ukweli kamili kuhusu suala hilo.

“Matokeo ya uchaguzi yatapingwa katika Mahakama ya Juu ili kubaini ukweli kuhusu suala hilo kwa manufaa ya Wakenya wote,” akaeleza.

Kwa upande wake, mgombea mwenza wa Bw Odinga Martha Karua amesema Dkt Ruto hawezi kuapishwa kabla ya kesi ambayo watawasilisha kusikizwa na kuamuliwa.

Akiongea jana katika kijiji cha Kiandieri, kaunti ya Kirinyaga alipohudhuria hafla ya mazishi ya Grace Wambui, Bi Karua alisema yeye na Bw Odinga sharti wapate haki.

“Haki ndio ngao na mlinzi wetu,” aliwaambia waombolezaji.

Bi Karua akiwataka wafuasi wa Azimio kudumisha amani wakati huu ambapo yeye na Bw Odinga wanasaka haki mahakamani.

Alisema muungano wa Azimio unataka Mahakama ya Juu kubaini nani halisi alishinda katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 ili Wakenya waridhike.

Hata hivyo kufikia jana, kundi la mawakili wa Azimio walikuwa wakiendelea kujiandaa kuwasilisha kesi hiyo katika mahakama hiyo inayoongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome.

Kisheria, Azimio ina muda wa hadi Jumatatu Agosti 22, 2022 kuwasilisha kesi hiyo. Kwa mujibu wa Katiba kesi hiyo inapasa kusikizwa na kuamuliwa ndani ya siku 14.

Hii ina maana kuwa uamuzi huo utatolewa rasmi mnamo Septemba 5, 2022

  • Tags

You can share this post!

Ushindi wa ODM Kwale kupingwa mahakamani

Shinikizo zazidi kwa Kalonzo ajiunge na Ruto

T L