• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Ujumlishaji kura Kieni waendelea IEBC ikitarajia shughuli hiyo itakamilika kesho Alhamisi

Ujumlishaji kura Kieni waendelea IEBC ikitarajia shughuli hiyo itakamilika kesho Alhamisi

NA SAMMY WAWERU

SHUGHULI ya kujumlisha kura eneobunge la Kieni, Kaunti ya Nyeri inaendelea siku moja baada ya taifa kushiriki uchaguzi mkuu, Agosti 9.

Zoezi hilo lilianza mapema Jumatano, na kufikia sasa foleni ya masanduku ya kura ambazo hazijajumlishwa ingali ndefu.

Linafanyika katika kituo kikuu cha kujumlisha kura, kilichoko Shule ya Upili ya Mweiga.

Eneobunge la Kieni lina idadi jumla ya vituo 232 vya kupigia kura.

Afisa wa IEBC anayesimamia shughuli hiyo (R.O), Bw David Mbui ameambia Taifa Leo huenda ikaendelea hadi kesho, Alhamisi.

Masanduku yote hata hivyo yamewasili.

Masanduku ya kura yakiwa yamepelekwa katika Shule ya Upili ya Mweiga ambapo ndipo kilipo kituo cha kujumlisha na kutangaza rasmi matokeo ya kura Kieni. PICHA | SAMMY WAWERU

Hayo yakiendelea, mbunge wa sasa Kieni, Kanini Kega amekubali kushindwa kuhifadhi kiti chake hata kabla ya matokeo rasmi kutangazwa na IEBC.

Bw Kega alitoa tangazo hilo kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, akisema “nimefungua chapta nyingine, mlango mmoja unapofungika mwingine hufunguka…”

Mbunge huyo anayeondoka aliwania kutetea wadhifa wake kupitia tiketi ya Jubilee.

Alimenyana na mgombea wa UDA, Wainaina Njoroge.

Kura zikiendelea kujumlishwa, zinaashiria Bw Njoroge huenda akatwaa kiti cha ubunge Kieni.

Hali ya usalama imeimarishwa Shule ya Upili ya Mweiga, vikosi vya pamoja vya askari vikishika doria kila pembe ya mazingira.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Kenya na Somalia ziimarishe vita dhidi ya...

Uchaguzi 2022: Ruto, Raila wafuatana kwa karibu kura...

T L