• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 7:55 PM
Wajackoyah kuvumisha biashara ya bangi, nyoka

Wajackoyah kuvumisha biashara ya bangi, nyoka

NA MWANDISHI WETU

INGAWA mwaniaji kiti cha Urais kwa tikiti ya chama chake cha Roots Party Prof George Wajackoyah ni mgeni katika siasa za humu nchini, amejizolea umaarufu kwa kutoa ahadi zake kwamba atahalalisha matumizi na uuzaji wa bangi au marijuana.

Prof Wajackoya anasema mauzo ya bhangi ndio suluhu ya matatizo ya kiuchumi yanayokumba nchi hii.

Prof Wajackoyah aliyekuwa akiishi uhamishoni Uingereza na Amerika ametambulika kwa kujifunga kitambaa na kujivika nguo za mitindo ya kipekee licha ya kuwa na umri wa miaka 63.

Prof Wajackoyah ambaye amemteua Bi Justina Wangui kuwa mwaniaji mwenza pia ameahidi kuvumisha ufugaji wa nyoka alizosema zitapata soko nchini Uchina.

Mapendekezo yake ya kuhalilisha mauzo ya bhangi nchini na ng’ambo amesema yataisaidia kupata fedha zitakazotumika kulipia deni la Sh10 trilioni.

Mwaniaji kiti huyu wa urais amesema siku yake ya kwanza katika Ikulu atetenga mahali maalum pa kuvutia bhangi kufukuza mapepo hata kabla ya kuhalalisha matumizi yake.

  • Tags

You can share this post!

Kinyang’anyiro 2022: Kaunti ya Lamu

Mwilu akemea ongezeko la ubakaji watoto

T L