• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Wamalwa ahimiza viongozi wa OKA wasiwe na ubinafsi

Wamalwa ahimiza viongozi wa OKA wasiwe na ubinafsi

Na OSBORNE MANYENGO

VIONGOZI wa Muungano wa One Kenya Alliance (OKA) kutoka eneo la Magharibi, wametakiwa kuacha ubinafsi na kuwahusisha viongozi wengine katika mipango yao.

Akihutubia waombolezaji mwishoni mwa wiki kwenye mazishi ya aliyekuwa chansela wa vyuo vikuu vya Egerton na Kabianga, Profesa Richard Musangi, Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa, aliwasuta viongozi hao wa ANC Musalia Mudavadi na Seneta wa Bungoma Moses Wetangula ambaye ni kinara wa Ford Kenya, kwa kutowahusisha.

“Tunasikia tu OKA na mimi kama mmoja wa viongozi kutoka eneo la Mulembe sijahusishwa. Sasa itakuwaje mnataka uongozi ilhali nyumba yenu yenyewe au boma hujaweka familia pamoja na unataka jirani akusaidie. Hayati Nelson Mandela alisema ukitaka kwenda safari ya mbali na ufike vizuri andamana na wenzako,” akasema.

You can share this post!

Franck Ribery ajiunga na Salernitana ya Italia akiwa na...

Kenya yapokea dozi 880,320 za chanjo aina ya Moderna