• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 5:50 AM
Siraj Mohamed sasa atia bidii kuichezea Harambee Stars

Siraj Mohamed sasa atia bidii kuichezea Harambee Stars

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

BEKI wa Bandari FC, Siraj Mohamed amesema anafanya bidii ya mazoezi ya kibinfasi kuhakikisha anacheza kiwango cha juu cha kumridhisha kocha wake Andre Cassa Mbungo pamoja na wakuu wa klabu yangu ya Bandari FC ili aweze kuhifadhi namba yake kwa timu.

Mohamed anasema mbali na kuridhisha timu yake, pia anajitahidi kucheza ili kumvutia kocha wa timu ya taifa ya Harambee Stars, Jacob “Ghost” Mulee amfikirie kumjaribu katika timu ya taifa ya Harambee Stars.

“Ni ndoto na matakwa ya kila mchezaji kuona amechaguliwa katika kikosi cha timu ya taifa nami sitakuwa kinyume. Nina hamu kubwa ya kuonekana kiwango cha uchezaji wangu ni kikubwa kinachoweza kunipa fursa ya kufanya majaribio timu ya taifa,” akasema Mohamed.

Mwanasoka anayewavutia mashabiki wa timu yake hiyo kwa jinsi anavyocheza vizuri hadi mara nyingimne kufanya  mbele na kutoa krosi safi mara kwa mara huku akiwa na uhakika wa kurudi nyuma kuwahi kuwazuia maadui, anasema nia yake kubwa ni kuwa katika kikosi cha Stars.

Alisema anaomba Mungu kumalizike kwa tatizo la virusi vya corona ili wapate kurudi viwanjani kukamilisha mechi zao za ligi ili waweze kupanda ngazi na ana matumaini makubwa kwa juhudi na wenzake, wataweza kumaliza nafasi ya kwanza ama tatu bora.

“Nina imani kubwa tukirudi uwanjani, timu yetu ya Bandari itaendelea kufanya vizuri chini ya mkufunzi wetu Mbungo. Nina hakika wachezaji wenzangu wote wanaendelea kufanya mazoezi ya kibinafsi ili ruhusa iikitolewa ya michezo kurudi, tutakuwa tuko sawa,” akasema Mohamed.

Mchezaji huyo ana imani kubwa Bandari itaendelea kuwa mojawapo ya klabu kubwa hapa nchini kwani wanasoka wake wanaichezea timu hiyo kwa ari ya kuipatia ushindi wakiwa na nia pia ya kufanikiwa kuwa timu ya pili ya Pwani baada ya Feisal FC mwaka 1965 kubeba taji la ligi kuu.

You can share this post!

Corona: Idadi ya waliopokea chanjo duniani yafika bilioni

Muturi na Lusaka wapokea ripoti kuhusu Mswada wa BBI