• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:50 AM
Uswidi wakomoa wenyeji Australia na kujizolea nishani ya shaba katika Kombe la Dunia

Uswidi wakomoa wenyeji Australia na kujizolea nishani ya shaba katika Kombe la Dunia

Na MASHIRIKA

WAREMBO wa Uswidi walijizolea nishani ya shaba na tuzo ya Sh376 milioni baada ya kupepeta wenyeji Australia 2-0 katika pambano la kutafuta mshindi nambari tatu lililopigiwa ugani Suncorp jijini Brisbane, Australia.

Mabao ya Uswidi yalifumwa kimiani kupitia kwa Fridolina Rolfo na Kosovare Asllani kunako dakika za 30 na 62 mtawalia. Kikosi hicho kiliambulia nafasi ya pili duniani mnamo 2003 na kujizolea medali ya shaba mnamo 1991, 2011 na 2019.

Australia waliotinga robo-fainali za Kombe la Dunia mnamo 2007, 2011 na 2015, walitia mfukoni kima cha Sh354 milioni.

Hadi kufikia mwaka huu, Australia walikuwa wametinga robo-fainali za Kombe la Dunia mara moja pekee (2015) na ndio wenyeji wa kwanza wa kutinga nusu-fainali za kipute hicho baada ya Amerika mnamo 2003.

Uswidi walianza kampeni za Kundi G kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Afrika Kusini kabla ya kulaza Italia (5-0) na Argentina (2-0). Walidengua mabingwa watetezi, Amerika, kwa penalti 5-4 baada ya sare tasa katika hatua ya 16-bora. Walipokeza Japan kichapo cha 2-1 kwenye robo-fainali kabla ya Uhispania kuwatandika 2-1 katika hatua ya nne-bora.

Kwa upande wao, Australia walianza kampeni zao za Kundi kwa ushindi 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland kabla ya kukubali kichapo cha 3-2 kutoka kwa Nigeria na kucharaza Canada 4-0.

Walipiga Denmark 2-0 katika hatua ya 16-bora kabla ya kufunga Ufaransa penalti 7-6 kufuatia sare tasa katika robo-fainali. Uingereza waliwapepeta 3-1 katika nusu-fainali.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Tanzia: Watu 6 wafariki asubuhi ya harusi

Budapest: Mtembeaji Gathimba akosa Sh720,000 kwa kumaliza...

T L