• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 5:46 PM
MAPISHI KIKWETU: Mchicha

MAPISHI KIKWETU: Mchicha

NA MARGARET MAINA

[email protected]

KITOWEO cha mchicha hupikwa kwa sufuria moja ambapo mwanzo mchicha uliokatwakatwa hupikwa na kisha kukorogwa kwenye kitoweo cha pilipili.

Unaweza kuongeza protini yoyote ya chaguo lako kama vile nyama, kamba, samaki mkavu, au samaki wengine wa chaguo kutegemea na matamanio yako.

Weka viungo vyako vyote pamoja: nyama iliyochemshwa, samaki, kuku, au chaguo jingine lolote la protini.

Pasha mafuta kwenye sufuria lililoinjikwa kwa chanzo cha moto wa wastani kisha ongeza vitunguu mara tu mafuta yanapochemka kiasi.

Kaanga pilipili iliyochanganywa kwa blenda. Utahitaji kukaanga hadi maji kwenye mchuzi yayeyuke na mchuzi kupunguka.

Tafadhali kumbuka kuwa makini na mchuzi ili usiungue. Hakikisha unakoroga kila mara hadi ufikie uthabiti huo mzito.

Ongeza viungo vyovyote upendavyo kisha ongeza nyama na mchicha: Mchuzi unapaswa kukolezwa wakati huu na viungo na vikolezo vyote hivyo.

Ongeza protini uliochagua. Acha iive ili iweze kuloweka utamu wote wa mchuzi. Kisha, koroga mchicha.

Rekebisha viungo ikiwa ni lazima. Ondoa kutoka kwa moto na upakue.

Vidokezo muhimu:

  • Unaweza kublanchi mchicha kabla ya kuongeza kwenye mchuzi – Unaweza kublanchi kwa kuongeza mchicha uliokatwakatwa kwenye maji na kuchemsha kwenye moto mwingi kisha uondoae kwenye moto mara moja unafikia kiwango chake cha kuchemka. Kisha mimina mchicha kwenye sahani na suuza chini ya maji baridi zaidi mara kadhaa ili kusimamisha mchakato wa kupika.
  • Wakati wa kaanga vitunguu, usiache viungue bali usubiri tu vigeuke na kuwa na rangi ya kahawia kiasi.
  • Kumbuka kumwaga maji mengi uwezavyo kutoka kwa mchicha kwani maji ya ziada kutoka kwa mchicha yanaweza kusababisha kitoweo chako kuwa na maji mengi.
  • Tags

You can share this post!

Ruto amwondoa Haji kama DPP

Idadi ya chui yapungua Maasai Mara

T L