• Nairobi
  • Last Updated February 28th, 2024 8:55 PM
Demu alia kukosa ‘nyota’ ya kupata dume la kumpa burudani chumbani

Demu alia kukosa ‘nyota’ ya kupata dume la kumpa burudani chumbani

Na JANET KAVUNGA

MOMBASA MJINI

KIPUSA mmoja mjini hapa aliwalilia wenzake wamsaidie akisema wanaume wamekuwa wakimtoroka punde tu anapoingia boksi.

Binti huyo alisema hajawahi kuwa na mpenzi wa kiume kwa zaidi ya mwezi mmoja japo angetaka kuwa na uhusiano wa dhati wa kimapenzi na hatimaye kuolewa.

“Huwa ninarushiwa mistari na wanaume lakini kila anayeteka moyo wangu, huwa ananiacha ninapomkubali, na baadhi huniacha hata kabla ya kuwafungulia mzinga waonje asali,” demu alisononeka katika ukurasa wa mtandao wa kijamii akiomba ushauri kutoka kwa wenzake.

Hata hivyo, wengi walimshauri ajifunze kuchangamsha wanaume na kutowapa masharti wapenzi hao huku wengine wakimtaka asiwe mwepesi wa kumeza chambo kwa kuwa machali hawapendi mademu wanaowakubali haraka.

  • Tags

You can share this post!

Watu 6,000 waangamia baada ya kimbunga kupiga eneo la...

Wakulima Homa Bay wasusia mbolea ya bei nafuu

T L