• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 8:55 PM
Mganga atisha kumdhuru mteja aliyeshindwa kukamilisha malipo ya kukingiwa boma

Mganga atisha kumdhuru mteja aliyeshindwa kukamilisha malipo ya kukingiwa boma

NA CORNELIUS MUTISYA

NZAIKONI, MACHAKOS

MGANGA mmoja alizua rabsha katika boma la buda mteja wake akidai malipo ya huduma.

Ilifichuka kuwa jamaa alialika mganga huyo nyumbani kwake kukinga boma lake asitatizwe na wachawi na akamlipa nusu ya ada za huduma.

Jamaa alipokosa kulipa salio ndani ya muda uliowekwa, mganga alifika nyumbani kudai.

“Nimekuja kupokea malipo na siachi ng’o!’’ mganga alifoka.

Mganga alitisha kumdhuru jamaa na familia yake iwapo hangemlipa pesa zake kisanga ambacho kilivutia baadhi ya majirani.

Inasemekana mganga alizua rabsha huku akifanya vimbwanga vyake na kumfanya jamaa kuogopa na kisha akamlipa pesa zake.

Mganga alimwambia jamaa kuheshimu kazi za watu.

  • Tags

You can share this post!

GWIJI WA WIKI: Dkt Timothy Kinoti

Bei ya pombe kuongezeka kwa asilimia 300 pendekezo la...

T L