• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Wanaume wa kupenda ndogondogo watiwa majaribuni kwa kutangaziwa bonasi

Wanaume wa kupenda ndogondogo watiwa majaribuni kwa kutangaziwa bonasi

NA MWANGI MUIRURI

GITHURAI 45

MSIMU wa shamrashamra za Krismasi na Mwaka Mpya huja na vituko vya kila aina.

Mnamo Desemba 17, 2023, baadhi ya vibiritingoma wanaoendesha shughuli zao katika eneo hili waliwatia wanaume wanaopenda ndogondogo majaribuni.

Hii ni baada ya kutangaza kwamba wateja wao watiifu katika biashara hiyo ya kutiliwa shaka maadili yake, kutangaza ‘bonasi’ ya siku tisa hadi 10 kwa wateja wao watiifu.

Mdokezi ambaye ni mmoja wa watoa bonasi hizo alisema afueni hiyo itatolewa kuanzia mkesha wa kuamkia Krismasi hadi siku ya kwanza Mwaka Mpya.

“Lengo ni kupalilia uhusiano mwema nao tukiingia Mwaka Mpya,” akasema mdokezi huyo.

Aidha mdokezi huyo pamoja na wenzake walidai hatua hiyo inalenga kuzima kasumba kwamba haja yao huwa ni kuvuna pesa na si watu wenye hisia.

Papo hapo mmoja wao akadai ndiyo maana hata “tunalaani kabisa hatua ya wengine miongoni mwetu kuwapora wanaosaka huduma za aina hii”.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi Rais Joe Biden alivyonusurika gari lilipogonga...

Mhadhiri katika chuo kikuu ashtakiwa kwa kuwadhulumu watoto...

T L