• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Adhabu ya kunyongwa yashtua washtakiwa  

Adhabu ya kunyongwa yashtua washtakiwa  

Na RICHARD MUNGUTI

WAVULANA wawili wa umri wa miaka 21 na 20 mtawalia Jumanne walipata mshtuko mkuu walipofahamishwa wakipatikana na hatia watatiwa kitanzi.

Newton Livoi (21) na Brian Ochieng walioshtakiwa kwa wizi wa mabavu “walihema huku wakitokwa na jasho mwendo wa saa tano asubuhi katika mahakama ya Milimani.”

Hakimu mkuu aliwatahadharisha Newton na Brian kwamba endapo watakiri shtaka adhabu itakayopitishwa ni kifo.

“Chini ya kifungo mlichoshtakiwa adhabu yake ni kifo. Hivyo basi makinikeni kabla ya kujibu,” hakimu mkuu Lucas Onyina aliwaeleza wavulana hao wa umri wa miongo miwili kila mmoja.

Wawili hao walikabiliwa na shtaka kwamba mnamo Aprili 23, 2023 mwendo wa saa 11 unusu wakishirikiana walimnyang’anya Peter Kariuki Munene simu aina ya Huawei P30 yenye thamani ya Sh18, 000.

“Mlimtishia maisha Munene mliponyang’anya simu na kutoroka nayo,” Onyina aliwaeleza washtakiwa.

Wawili hao waliikanusha shtaka na kuomba mahakama iwaachilie kwa dhamana.

Kiongozi wa mashtaka Anderson Gikunda hakupinga ombi hilo ila alieleza korti izingatie adhabu kali itakayopitishwa washtakiwa wakipatikana na hatia.

Bw Onyina aliamuru idara ya urekebishaji tabia iwasilishe ripoti kuwahusu washtakiwa kabla ya kuwaachilia kwa dhamana.

Kesi itatajwa baada ya wiki mbili kutengewa siku ya kusikizwa.

  • Tags

You can share this post!

Wanafunzi 8,000 wanufaika na hundi za basari Starehe

Serikali za kaunti zadai mabilioni, shughuli za kaunti...

T L