• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 8:55 PM
Afueni bei ya kahawa ikiimarika

Afueni bei ya kahawa ikiimarika

Na GERALD ANDAE

MAPATO ya kahawa katika mwaka wa kifedha wa 2019/2020 yameongezeka kwa asilimia 52.

Ongezeko hili lilitokana na ongezeko la mahitaji ya kahawa ya Kenya baada ya zao hilo nchini Brazil kupungua kwa sababu ya hali mbaya ya anga.

Soko la Kahawa la Nairobi (NCE) lilisema kuwa Kenya ilipata Sh15.2 bilioni kwa mauzo ya kahawa katika mwaka ulioisha Septemba 30.

Ikilinganishwa na mwaka wa 2019, bei ya gunia ya kilo 50 iliongezeka kutoka Sh20,412 hadi Sh30, 348 mwaka 2020.

“Bei ya juu ambayo tulishuhudia, imewezesha thamani ya kahawa inayouzwa kuongezeka kwa asilimia 52.27 katika mwaka wa 2020/2021 ikilinganishwa na ile ya mwaka wa 2019/2020,” NCE ikasema.

Vile vile, ongezeko hili lilitokana na bei ya juu ya kimataifa ambayo ilifikia pauni Sh33,984 toka 2012 sababu ya hali mbaya ya anga nchini Brazil.

Nchi ya Brazil ni moja kati ya nchi ambazo hutoa kahawa nyingi duniani.

Nchi hiyo hutoa kilo 60 milioni za Kahawa kila mwaka lakini baridi imeifanya ipoteze asilimia 20 ya mmea huo wakati huu na kusababisha upungufu wa kahawa katika soko duniani.

Hivi majuzi, Benki Kuu ya Kenya (CBK) ilikuwa imetabiri ongezeko la bei ya Kahawa ya Kenya katika soko la kimataifa kufuatia kupungua kwa kahawa ya Brazil.

Gavana wa CBK, Dkt Patrick Njoroge alisema kuwa Kenya ingenufaika kutokana na hali mbaya ya anga inayoikumba Amerika Kusini na inayoathiri uzalishaji wa kahawa.

“Hivi majuzi kumekuwepo na ongezeko la bei ya kahawa duniani linalotokana na baridi inayoshuhudiwa Brazil na tunaweza tukanufaika kwa kuongeza bei ya kahawa kwenye soko,” akasema Dkt Njoroge wakati wa kuzindua ripoti ya Kamati ya Sera za Pesa.

  • Tags

You can share this post!

Waiguru apata marafiki wapya baada ya kukumbatia Naibu Rais

Zuleikha apinga ushindi wa Mwanyoha uenyekiti ODM