• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 8:55 PM
Baadhi ya changamoto za wanafunzi katika mitaa ya mabanda

Baadhi ya changamoto za wanafunzi katika mitaa ya mabanda

NA SAMMY KIMATU

MKAKATI wa serikali kuhakikisha wanafunzi wote wanaokamilisha elimu ya msingi wanajiunga na sekondari umefeli kwenye maeneo ya Mukuru katika tarafa ya South B, kaunti ndogo ya Starehe.

Starehe ina wadi mbili, Landi Mawe na Nairobi South.

Watoto wengi kutoka katika mitaa ya mabanda.

Katika wadi ya Nairobi South, shule ya upili ya kutwa ni moja na haiwezi kudhibiti idadi kubwa ya wanafunzi kutoka Mukuru.

Akiongea na Taifa Leo mnamo Jumanne, naibu chifu eneo la Hazina Bw Vincent Ambuga alikiri kwamba wanafunzi wengi hulazimika kukaa nyumbani kutokana na ukosefu wa karo.

Bw Ambuga aliongeza kwamba licha ya karo ya sekondari kupunguzwa na serikali kuwa kati ya Sh7,000 na Sh10,000 kwa mwaka, pesa hizo bado ni nyingi kwa baadhi ya wazazi.

Mbali na Bw Ambuga, machifu na maafisa wengine wa utawala katika kaunti ndogo ya Starehe, wanasema kwamba wazazi hawawezi kugharimia karo za watoto wao kutokana na uchochole.

“Shule ya upili ya Nairobi South ndiyo ya pekee ya serikali na iliyo ya kutwa katika tarafa ya South B. Watoto katika mitaa ya mabanda ya Mukuru ni wengi kuliko nafasi za watoto shuleni,” chifu Ambuga akasema.

Kando na hayo, katika tarafa ya Viwandani kuliko na mitaa mingi ikiwemo Mukuru-Lunga Lunga, Mukuru-Paradise na Mukuru-Jamaica miongoni mwa mingine, ni shule ya sekondari ya Star Of Hope pekee iliyo ya kutwa na ya serikali.

Shule mbadala nyingine ya serikali na iliyo ya kutwa ni Shule ya Upili ya Makongeni licha ya kuwa mbali na wakazi mitaa ya Mukuru.

Naibu Mkurugenzi wa Mukuru Promotion Centre (MPC) Bi Dinah Mwendwa aliambia Taifa Leo kwamba ukosefu wa kazi uliochangiwa na janga la corona uliyumbisha wengi.

“MPC huwa na shule nne za msingi na moja ya upili kwa watoto karibu 7,000 kutoka maeneo ya Mukuru. Lishe kwa watoto hao wote hugharimiwa na wadhamini wetu-Team Pankaj ikishirikiana na MPC,” Bi Mwendwa akasema.

  • Tags

You can share this post!

KDF: Nembo ya utu kwa raia wema

Walinzi wa Fernandes Barasa watiwa mbaroni kwa kushambulia...

T L