• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:50 AM
Babu Owino akana madai kwamba alichochea fujo Jacaranda

Babu Owino akana madai kwamba alichochea fujo Jacaranda

NA CHARLES WASONGA

MBUNGE wa Embakasi Mashariki Babu Owino amejitenga na madai kuwa alichochea vurugu zilizoshuhudiwa katika uwanja wa Jacaranda, Nairobi kabla ya mkutano wa muungano wa Kenya Kwanza, Jumapili, Juni 19, 2022.

Kupitia ujumbe katika akaunti yake ya Twitter, Bw Owino alidai kuwa fujo hizo zilizochangia watu watano kujeruhiwa zilipangwa kimasukudi na muungano huo wa Kenya Kwanza.

Mbunge huyo alichapisha picha ambazo alidai ni ushahidi kwamba hakupanga machafuko hayo yaliyochangia kujeruhiwa kwa mgombea ubunge kwa tikiti ya chama cha United Democratic Alliance (UDA) Francis Mureithi aliyepata jeraha kichwani.

“Tazama picha hizi kwa makini. Watu wenye sare za UDA ndio walishambulia gari la Ruto kwa mawe. Ni wao ndio waligeuka na kujifanya kutoa usalama katika mkutano huo. Msituhadae baada ya kupanga mashambulio dhidi yenu,” Owino akasema.

Kauli ya Mbunge huyo ilijiri baada ya mgombea urais wa Kenya Kwanza Naibu Rais William Ruto kudai mshindani wake mkuu Raila Odinga ndiye alichochea ghasia hizo.

Akiongea katika uwanja huo wa Jacaranda, Dkt Ruto alidai kuwa mgombea huyo wa urais wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya aliwakodi vijana kuzuia kusambaratisha mkutano huo kwa lengo la kuwatisha wafuasi wake.

“Hakuna vitisho, vitendo vya urushaji mawe au kutumiwa kwa vijana kutatuzuia kushinda uchaguzi mkuu wa Agosti 9,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Jubilee Mlimani waomba Raila msamaha na kuahidi kumpigia...

CUE yamtaka Sakaja ajue haifanyi masihara

T L