• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 8:55 PM
Bunge la Uganda lafungwa kwa wiki mbili kutokana na makali ya corona

Bunge la Uganda lafungwa kwa wiki mbili kutokana na makali ya corona

BUNGE la Uganda litafungwa kwa wiki mbili kupisha maafisa wa afya kunyunyizia jengo la bunge dawa ya kuua virusi vya corona.

Wabunge hawataruhusiwa kufika katika majengo ya bunge kati ya Juni 28 na Julai 11, mwaka huu, kulingana na taarifa iliyotolewa Jumanne na karani wa bunge Jane Kibirige.Hatua hiyo inafuatia baada ya watu 100, wakiwemo wabunge na wafanyakazi wa bunge, kuambukizwa virusi vya corona.

“Bunge la Uganda, sawa na maeneo mengine ya nchi, limeathiriwa pakubwa na wimbi la pili la ugonjwa wa corona,” akasema Kibirige.Kufikia Jumanne, Uganda ilikuwa imethibitisha visa 73,401 vya walioambukizwa virusi vya corona.

Watu 714 wameaga dunia kutokana na maradhi hayo.Wakati huo huo, nchi jirani ya Rwanda imeonya kuwa serikali inapanga kupiga marufuku watu kutoka katika makazi yao endapo wataendelea kupuuza masharti yaliyowekwa kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Waziri wa Afya Daniel Ngamije jana alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona nchini humo tangu Juni 8, mwaka huu.Serikali Jumatatu, ilipiga marufuku sherehe zote za harusi.

“Ongezeko hilo la maambukizi ni ishara kwamba watu wameanza kupuuza masharti yaliyowekwa kama vile kuepuka sehemu zilizo na misongamano, kunawa mikono mara kwa mara na kuvalia barakoa,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Aina mpya ya virusi vya corona yaibua hofu India

Handisheki ni matunda ya uongozi mbaya – Mutua