• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 8:55 PM
Chiloba awatahadharisha Wakenya wasipokee simu kiholela

Chiloba awatahadharisha Wakenya wasipokee simu kiholela

NA NDUBI MOTURI

MAMLAKA ya Mawasiliano nchini imeonya Wakenya kuhusu wimbi jipya la ulaghai kupitia simu za mkononi uliobandikwa jina ‘wangiri’.

Wahalifu hao sasa wanatumia ujanja wa kuwapigia watu simu wakitumia nambari ya nchi za kigeni na baadaye kukata simu.

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Ezra Chiloba, amewaonya Wakenya dhidi ya kupokea simu ikiwa hawamtambui anayepiga.

“Hapa nchini Kenya, simu zinazohusika kwenye sakata hiyo ni za kodi +51(Peru), +64(New Zealand) miongoni mwa nyinginezo,” amesema Bw Chiloba.

Amesema mpokeaji simu ambayo inakatwa mara moja anashawishika kumpigia aliyepiga mwanzo. Hapo ndipo simu inaelekezwa kwa nambari tofauti ambayo iko kwa mfumo wa kutoa huduma za kulipia, kumaanisha kwamba salio la muda wa maongezi hukatwa.

  • Tags

You can share this post!

Baraza la kusimamia biashara ya vyuma chakavu laonya...

Madhehebu: Kamati teule kupendekeza Bunge libuni sheria...

T L