• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Chipukizi Appiah aanza kuona matunda ya uigizaji

Chipukizi Appiah aanza kuona matunda ya uigizaji

Na JOHN KIMWERE 
PENYE nia pana njia.
Ndivyo wahenga walivyologa, tangia zama zile baada ya kupasua hilo mpaka sasa, msemo huo ungali na mashiko siyo haba miongoni mwa jamii kwa jumla. Mercy Adhiambo Abok ni kati ya wasanii wanaokuja kwa kasi katika tasnia ya uigizaji huku wakilenga kutinga upeo wa kimataifa.
Kisura huyu ambaye kwa jina la msimbo anafahamika kama Appiah pia ni mwanamitindo na mwanafunzi wa mwaka wa pili kwenye chuo cha Daystar. Binti huyu  ambaye ndio amejiunga na chuo hicho amepania kuhitimu kwa shahada ya digrii kama mwana habari.
”Nilianza kuvutiwa na uigizaji nikiwa mdogo lakini nilianza kushiriki kama taaluma yangu miaka mwili iliyopita,” amesema na kuongeza kuwa ni muda chache lakini kiasi ameona matunda ya uigizaji.
Anasema alitamani kujiunga na uigizaji akisoma darasa la saba alipotazama filamu iitwayo Princess Tyra ya msanii Jackie Appiah mzawa wa Ghana. Ndani ya muda mchache dada kipusa huyu anajivunia kushiriki filamu kadhaa ikiwamo Country Queen iliyopata mpenyo na kupeperushwa kupitia Netflix.
Pia Kuna iliyopeperushwa kupitia Maisha Magic plus. Aidha zipo Shembu, Volume na Love me. Katika kipindi hicho amefanya kazi na makundi tofauti kama Good karma Fiction, Tililiz Pictures, Zamaradi Productions, Zena Bahati Production, Primary Pictures, Moremedia na Zidi Media.
Mercy Adhiambo Abok maarufu Appaih…Picha/JOHN KIMWERE
Dada huyu anasema kuwa binafsi huwa anahisi furaha tele anaposhiriki uigizaji anakosema kwamba analenga kutumia uigizaji kutoa funzo kwa jamii. Binti huyu aliyezaliwa mwaka 1997 anasema katika uigizaji analenga kufuata nyayo zake Jackie Appiah ambaye kwa wanawake hufanya kazi yake kwa kujituma mithili ya mchwa.
”Kenya tumekosa kutoa hadithi nzuri kama ilivyo katika mataifa mengine kama Amerika, Afrika Kusini, Mexico na India kati ya mengine,” alisema na kuongeza kuwa ndio sababu kubwa imechangia wananchi kutovutiwa na filamu za humu nchini.
Tangia akiwa mtoto kando na kuwa alipania kuhitimu kuwa mwigizaji pia alitamani kuwa mtangazaji kwenye runinga ambapo alikuwa akivutiwa na mtangazaji aliyekuwa akivuma nyakati hizo Esther Arunga (KTN).
Anasisitiza kuwa serikali inastahili kuunga mkono wasanii wote bila kubagua wale maarufu na wanaoibukia.
PANDASHUKA
Chipukizi huyu anadokeza kuwa sekta ya uigizaji imejaa pandashuka ambapo binafsi kwa zaidi ya miaka 20 amekosa ajira kwa kutokubali kuwa na mahusiano ya kimapenzi na maprodusa.
”Dah! bila kuongezea kachumbari maprodusa wengi tu wamekuwa na mtindo huo kunishawishi kuwa wapenzi ndipo nami wanipe ajira ya kuigiza,” akasema na kutoa wito kwa wenzake kuwa kamwe wasijishushe dhamana yao.
Pia anatoa wito kwa maprodusa waache mtindo wa kudharau wasanii wengine kwa misingi ya maumbile hasa kupuuza wale wenye ngozi weusi kama yeye.
Mercy Adhiambo Abok maarufu Appiah..Picha/JOHN KIMWERE
  • Tags

You can share this post!

FAUSTINE NGILA: Safaricom ikomeshe teknolojia ya kidole kwa...

Joylove inataka kushiriki kipute cha CAF miaka ijayo

T L