• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Dereva atozwa faini ya Sh70000 kwa kumuua mwanafunzi

Dereva atozwa faini ya Sh70000 kwa kumuua mwanafunzi

Na RICHARD MUNGUTI

POLISI waliochunguza kesi ambapo dereva wa gari ndogo alimgonga dafrau mwanafunzi na kumuua kisha akatozwa faini ya Sh70,000 wanaomba afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) ikate rufaa kwa vile adhabu iliyopitishwa hailingani na kosa alilofanya.

Rodgers Omondi Ochomo aliyekabiliwa na mashtaka mawili ya kusababisha kifo kwa kuendesha gari bila makini na kumjeruhi mwanafunzi alihukumiwa na hakimu mkazi Bw Philip Mutua.Kwa makosa hayo mawili mshtakiwa alitozwa faini ya Sh50,000 kwa kusababisha kifo cha mwanafunzi kwa kuendesha gari bila makini.

Atatumikia kifungo cha miezi 12.Kwa kosa la kumjeruhi mwanafunzi mshtakiwa alitozwa faini ya Sh20,000 ama atumikie kifungo cha miezi sita.Kwa  jumla alitozwa faini ya Sh70,000 ama atumikie kifungo cha miezi 12.Mahakama iliamuru dhamana ya pesa tasilimu ya Sh100,000 aliyokuwa amelipa mshtakiwa itumikie kulipia faini hizo.

Ochomo alilipa faini hiyo mara moja na kutoka akiwa huru. Pia alirudishiwa Sh30,000 baada ya kulipa faini hiyo.Lakini maafisa waliochunguza kesi hiyo walilalamika na kuambia Taifa Leo “adhabu aliyopata Ochomo hailingani na makosa aliyotenda ya kusababisha kifo na majeraha. DPP anapasa kukata rufaa.”

Akijitetea baada ya kupatikana na hatia ya kusababisha kifo kwa uendeshaji mbaya wa gari,Ochomo alisema “ameteseka baada ya kupoteza kazi kufuatia ajali hiyo.Aliomba msamaha na kuahidi kuwa makini siku za usoni.”Mbali na kumuua mwanafunzi huyo Ochomo alimjeruhi mwingine.

Siku hiyo alisababisha kifo hicho magari mengine yalikuwa yamesimama wanafunzi wavuke lakini mshtakiwa akafululiza gari aliyokuwa akiendesha na kusababisha maafa hayo.Alikuwa amesimamishwa pia na dereva wa shirika la kulinda wanyama mwituni (KWS)

  • Tags

You can share this post!

Mwanachama wa Mungiki atisha kuua landilodi

Chama kipya Pwani kinavyotishia Ruto na Raila