• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 6:55 PM
Droo ya Cecafa U23 kufanywa kupitia Zoom mnamo Ijumaa

Droo ya Cecafa U23 kufanywa kupitia Zoom mnamo Ijumaa

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya soka ya wanaume ya Kenya ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 maarufu kama Emerging Stars, itafahamu wapinzani wake wa makundi ya dimba la Cecafa mnamo Juni 25.

Mkurugenzi wa Muungano wa Mashirikisho ya Soka ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Auka Gacheo alieleza wanachama 11 wa muungano huo kuwa droo itafanywa kupitia mtandao wa Zoom hapo Ijumaa.Mashandano haya yatafanyika mjini Bahir Dar nchini Ethiopia mnamo Julai 13-18.

Sheria za mashindano hayo zinahitaji mchezaji kuwa amezaliwa Januari 1 mwaka 1998 ama baadaye. Umri wa chini lazima uwe miaka 18 kufikia mwisho wa mwaka 2021. “Kila timu itakubaliwa kuwa na wachezaji watatu waliozidi umri wa miaka 23 katika mashindano hayo yatakayofungua msimu wa Cecafa,” afisa huyo Mkenya alisema.

Kufikia Juni 21, wanachama wote wa Cecafa isipokuwa Rwanda na Somalia, walikuwa wamethibitisha kushiriki.Katibu wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) Regis Uwayezu alieleza tovuti ya Cecafa kuwa kufikia Juni 23 usiku watakuwa wameingia mashindano hayo.

Wenyeji wa makala yaliyopita Uganda waliibuka washindi. Mataifa ambayo yamethibitisha kuwania taji la Cecafa U23, ni Uganda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Sudan, Sudan Kusini, Djibouti, Tanzania, Zanzibar, Kenya na wageni DR Congo.

  • Tags

You can share this post!

Waiguru aitaka Hazina ya Kitaifa kutoa fedha za Mei na Juni...

Hofu huenda Hyundai isiwezane na barabara za Safari Rally