• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 5:30 PM
Huyu anataka tupime ilhali niliokuwa nao walichovya bila kinga

Huyu anataka tupime ilhali niliokuwa nao walichovya bila kinga

SHANGAZI,

Nimepata mwanamume mpenzi wa dhati aliye tayari kuwa mwenzangu maishani. Lakini kuna changamoto. Anasisitiza tupimwe lakini naogopa kwa sababu nimekuwa na wapenzi kadhaa ambao walichovya asali bila kinga. Nishauri.

Siku hizi hiyo imekuwa tahadhari ya lazima kwa wapenzi wanaothamini maisha yao. Hiyo ni fursa nzuri kwako kujua hali yako ya afya kwa manufaa yako na mpenzi wako. Ukikataa atakushuku na labda kubadili nia yake kuhusu uhusiano wenu.

Mwanadada aliyeniomba pesa za dharura sasa aniambia nimkome!

Kuna mwanamke tuliyekutana juzi katika maskani ya starehe na tukapendana. Aliniomba pesa kushughulikia jambo la dharura na nikampa. Jana alinitumia ujumbe akaniambia nimkome eti ni mke wa mwenyewe. Nifanyeje?

Mwanamke huyo alitaka kukupora pesa tu na ndiyo maana alikubali ombi lako mara moja. Labda hata si mke wa mtu, hiyo ndiyo kazi yake. Usikate tamaa, hatimaye utapata mpenzi wa dhati.

Amebeba mimba yangu lakini hataki nimuoe

Mpenzi wangu ana mimba yangu na nimeamua kumuoa. Lakini amekataa akisema anahitaji muda zaidi kufikiria. Simuelewi kwa sababu amekuwa akiniambia ananipenda.

Uamuzi wa mpenzi wako unatia shaka. Pendekezo la ndoa linafaa kutoka kwake kwa sababu anabeba mtoto wako. Kama anakupenda anataka kufikiria nini? Kuna uwezekano mkubwa kuwa hataki kuwa mke wako. Kuwa tayari kwa chochote kile.

Nafaa kusubiri muda gani kuthibitisha ikiwa kweli ananipenda?

Nina mpenzi na matumaini yangu ni kuwa hatimaye atakuwa mke wangu. Nimekuwa naye kwa miaka miwili sasa na nataka kuhakikisha ananipenda kwa dhati. Je, ninafaa kusubiri kwa muda gani?

Inaweza kuchukua miezi au miaka kadhaa kuthibitisha mapenzi ya dhati. Wapenzi wanapokubaliana kufunga ndoa huwa wamefikia kilele cha mapenzi yao na hatua hiyo ni thibitisho la mapenzi ya dhati.

  • Tags

You can share this post!

Maafisa wa NIS washtakiwa kunyang’anya mfanyabiashara...

Bei ya mafuta yapaa juu zaidi

T L