• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Jamii yashtuka radi kupiga na kuua mke na mume, kujeruhi watu wengine watatu

Jamii yashtuka radi kupiga na kuua mke na mume, kujeruhi watu wengine watatu

Na JESSE CHENGE

[email protected]

Wanandoa kutoka eneo bunge la Malava, Kaunti ya Kakamega wamefariki baada ya kupigwa na radi Jumapili Septemba 9, 2023 jioni.

Wengine watatu, ikiwa ni pamoja na kijana mmoja, wamelazwa katika hospitalini wakiwa na majeraha mengi.

Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Musungu katika eneo bunge la Malava, Kaunti ya Kakamega ambapo nyuso zao zinaeleza hadithi ya jamii iliyogubikwa na huzuni nyingi kufuata kifo cha Nahashon Mwisukha, 51, na mkewe Margaret Munyelele mwenye umri wa miaka 44.

“Lilikuwa tukio la kushangaza sana, wawili hao, baba na mama. Radi ilikuja na kuwachukua wote wawili,” alisema Mulunda Lubale, mmoja wa majirani.

Kwa mujibu wa mashahidi, Margaret ambaye alikuwa ameungana na waumini wengine wa Kanisa la Africa Divine nyumbani kwao kwa sala, alitoka nje kumchukua mtoto wao, na alipokuwa akirudi ndani ya nyumba, alipigwa na radi.

Mume wake tayari alikuwa ndani ya nyumba.

Familia za waathirika, pamoja na jamii ya eneo hilo, zimeshangazwa na kushtushwa na tukio hilo la kuhuzunisha. Nahashon na Margaret inasemekana walikuwa watu wenye moyo wa huruma ambao waliishi maisha ya amani na walichangia kikamilifu katika jamii yao. Walikuwa vielelezo katika kanisa lao.

“Tukio hili lenye kuvunja moyo linatukumbusha kwa uchungu umuhimu wa kuelewa hatari za asili na kuchukua hatua za kuzuia majanga kama haya,” walisema viongozi wa kanisa.

“Tunatoa rambirambi zetu kwa familia na marafiki wa waathirika na tunatuma sala zetu kwa wale wanaouguza majeraha hospitalini”.   

  • Tags

You can share this post!

Wito jamii ishughulikie afya ya akili visa vya watu kujiua...

Polo wa kila mara ‘nionje kidogo’ abugia mkojo...

T L