• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Jinsi mahabusu wanawake walimwokoa Babu Owino ‘kuozea’ seli Wang’uru

Jinsi mahabusu wanawake walimwokoa Babu Owino ‘kuozea’ seli Wang’uru

Na MWANGI MUIRURI 

Julai 20, 2023 na Mbunge wa Embakasi Mashariki yuko katika kituo cha polisi cha Wang’uru kilichoko katika Kaunti ya Kirinyaga.

Akiwa ndani ya seli asubuhi hiyo, ambapo alikuwa amefungiwa peke yake baada ya kushukiwa kushiriki njama za maandamano na ghasia, aliomba usaidizi aoge.
 Kwa kuwa bafu ya seli hizo huwa kwa kona karibu na seli za wanawake, Bw Owino alipewa maji yaliyokuwa ndani ya ndoo.
 Mbunge huyo aliachwa peke yake akaoge kwa kuwa hakuna vile angetoroka.
“Hakuna kwingine angetokea ila tu kwa mlango wa kuzuia mahabusu na ambao ulikuwa umefungwa na pia askari wa kutosha kushika doria nje,” ripoti ya kituo hicho kwa tume ya huduma ya polisi (NPS) ya Julai 23 yaonyesha.
 Ripoti hiyo iliitishwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Bw Japhet Koome ikitaka maafisa wa Kituo hicho cha Wang’uru kuelezea jinsi Siri ya serikali ilifichuka na ikajulikana na familia na mawakili wake alikokuwa amefungiwa.
 Baada ya Bw Owino kuachwa akaoge, alipitia karibu na seli ya kinamama na ambao alisikia wakiwasiliana kwa simu wakiwa mahabusu.
 Kikatiba, inakubalika mahabusu kupewa simu kama haki yao ya kuwasiliana na wateule katika ulimwengu wa walio huru.
 Haki hiyo ambayo Bw Owino alikuwa amenyimwa lakini ikapewa mahabusu ndani ya seli hiyo ndiyo alinyakua na akapeana nambari ya simu ya mke wake apigiwe na aarifiwe mumewe alikuwa ‘anaozea’ seli za Wang’uru.
“Hivyo ndivyo Bw Owino alifanikiwa kuvunja usiri wa kutoweka kwake katika seli za stesheni yetu na kukazuka vurumai wakati mke wa mbunge huyo alifika akiandamana na raia wengine, mawakili na pia waandishi wa habari wakafuata na hali ikawa ya dharura,” ripoti hiyo ya Siri yaonyesha.
  • Tags

You can share this post!

Serikali ya Mung’aro yapata tiba ya kuzuia mauaji ya...

Dereva na msaidizi wake wauawa na Al-Shabaab katika eneo la...

T L