• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 11:37 AM
Serikali ya Mung’aro yapata tiba ya kuzuia mauaji ya wazee

Serikali ya Mung’aro yapata tiba ya kuzuia mauaji ya wazee

NA ALEX KALAMA 

SERIKALI ya Kaunti ya Kilifi imeanza kutekeleza mikakati yake ya kuhakikisha wazee wanalindwa dhidi ya mauaji na dhuluma za aina yoyote, mojawapo ya njia hizo ikiwa ni kuhakikisha vijana wa kaunti hiyo wanapewa ajira ili kuimarisha maisha yao.

Kulingana na Afisa Mkuu wa kitengo cha Vijana na Michezo, Naphtali Owino, serikali ya Kaunti ya Kilifi inapanga kuajiri vijana wengi katika mwaka huu wa kifedha ili kudumisha usafi katika kila sehemu za kaunti hiyo ikiwemo kwenye fuo za Bahari na mijini kama mmojawapo wa mipango ya kuzuia visa vya mauaji ya wazee.

Afisa Mkuu wa kitengo cha Vijana na Michezo katika Kaunti ya Kilifi, Naphtali Owino akihutubu. PICHA | ALEX KALAMA

Bw Owino anayefanya kazi chini ya Waziri wa Jinsia, Huduma za Kijamii na Masuala ya Vijana katika Kaunti ya Kilifi Dkt Ruth Dama, alifichua kwamba Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwanong’onezea mazuri yanayowalenga vijana.

Mpango huo utatekelezwa chini ya kaulimbiu ya ‘Ujuzi wa Kuhifadhi Mazingira kwa Vijana Kufanikisha Maendeleo Endelevu Duniani’.

“Sasa sisi tutawacha wazee watusaidie kimila lakini sisi tutafanya juhudi kuhakikisha mazingira yetu ni safi kutoka kwa bahari mpaka kwenye viwanja vya michezo,” akasema Bw Owino.

Wakati huo huo afisa huyo alisema kuwa kaunti inapanga kuandaa mashindano ya michezo na talanta mbalimbali ili kuhakikisha kuwa vijana wanakuza talanta zao.

“Pia tuko na mikakati ya kuhakikisha tunakuza vipaji Kilifi. Kwa hivyo, hivi karibuni tutaandaa matamasha mbalimbali ili kusaidia vijana kukuza vipaji vyao,” alisema Bw Owino.

Afisa Mkuu wa Maswala ya Vijana na Michezo katika Kaunti ya Kilifi Naphtali Owino. PICHA | ALEX KALAMA

Ikumbukwe ya kwamba Kaunti ya Kilifi ni mojawapo ya zile kaunti ambazo zimekuwa zikishuhudia visa vya mauaji ya wazee kwa tuhuma za uchawi.

  • Tags

You can share this post!

Al-Shabaab wateketeza Kanisa, nyumba 8 kijijini Salama

Jinsi mahabusu wanawake walimwokoa Babu Owino...

T L