• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 4:39 PM
Jinsi mfanyabiashara alivyojinasua kutoka kwa ‘mchele babe’ Kasarani

Jinsi mfanyabiashara alivyojinasua kutoka kwa ‘mchele babe’ Kasarani

JOSEPH NDUNDA na FRIDAH OKACHI

MFANYABIASHARA aliyedaiwa kumwekea mpenziwe dawa za kulevya kwenye kinywaji wakiwa katika chumba cha mapumziko eneo la Kasarani, Nairobi, ameshtakiwa kwa nia ya kumuibia kinyume na kifungu cha 230 cha Kanuni ya Adhabu.

Linet Kainyu, 32, anashtakiwa kwa kumpa Jacob Kibet dawa isiyotambulika mnamo Oktoba 23, 2023, baada ya kumwalika kunywa pombe na kufurahia maisha nyumbani kwake.

Kibet aligundua tembe hiyo kwenye kinywaji chake kabla ya kunywa na kutoroka chumbani humo kabla ya kuripoti kisa hicho kwa wasimaminzi wa nyumba hiyo na polisi.

Tembe hiyo inafanyiwa uchunguzi na wataalamu wa serikali kutambuliwa kabla ya kutumika kama ushahidi.

Bi Kainyu, anakabiliwa na shtaka jingine la kutoa taarifa za uongo za kupeana jina ambalo si sahihi kwa maafisa wa polisi baada ya kutiwa mbaroni.

Alifahamisha afisa wa polisi Kennedy Otieno, kwenye kituo cha polisi cha Kasarani kwamba jina lake lilikuwa ni Faith Makena ila kitambusho cha kitaifa lilitofautiana na lile lililoandikishwa kwenye kitabu cha matukio (OB).

Bw Kibet alikutana na Kainyu kwenye mkahawa na kumuomba simu yake ili amtafute dadake aweze kumtumia pesa za kulipa bili kwa kuwa simu yake ilikuwa imezimika.

Hata hivyo, Bw Kibet aliondoka kwenye meza waliokuwa wameketi pamoja na kuhamia kwenye sehemu nyingine na kununua vinywaji vingine kabla ya kuondoka.

Siku mbili baadaye, Kainyu alimpigia simu akimuomba wakutane kunywa pombe kwenye sehemu waliokutana awali.

Baada ya kukutana, wawili hao walinunua vinywaji kwa pamoja na kufanya uamuzi wa kuondoka na vinywaji vingine ili waelekee nyumbani.

“Kabla ya kulala, nilienda msalani na niliacha pombe yangu kwenye meza. Wakati niliporudi, nilikunywa kinywaji kile na kuhisi ulimi wangu ukiwa tofauti na kutema kwenye karatasi shashi. Niligundua nimewekewa dawa ya kulevya,” alisema Bw Kibet.

Aligundua amelewa na dawa za kulevya na akaarifu wasimamizi wa ghorofa hiyo ambao waliita maafisa wa polisi wamkamate Kainyu.

Mshukiwa alifikishwa katika Mahakama ya Makadara baada ya uchunguzi na kukanusha mashtaka mbele ya Hakimu mkuu Erick Mutunga.

Kainyu aliachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000 bila kupewa dhamana ya pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa Desemba 5 kabla ya kuanza kusikilizwa Aprili 4, 2024. 

  • Tags

You can share this post!

Mchezo wa paka na panya ‘kanjo’ wakitekeleza...

‘Mume wangu analea watoto wetu watatu, lakini hajui...

T L