• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 11:13 AM
‘Jungle’ Wainaina aeleza jinsi Njonjo alivyokuwa mwanasheria wa kipekee

‘Jungle’ Wainaina aeleza jinsi Njonjo alivyokuwa mwanasheria wa kipekee

Na LAWRENCE ONGARO

WAKAZI wa kaunti ya Kiambu, wameachwa na huzuni tele baada ya kupokea habari za kutokea kwa kifo cha mwanasheria shupavu, Sir Charles Mugane Njonjo.

Mbunge wa Thika Bw Patrick ‘Jungle’ Wainaina ametaja marehemu kama mwanasheria shupavu.

“Marehemu Njonjo wakati wa uhai wake alilinda katiba ya nchi yetu kwa weledi wa hali ya juu,” amesema Bw Wainaina.

Mbunge huyo amesema hadi wa leo pengine hakuna mtumishi wa serikali katika upande wa sheria anayeweza kulinganishwa na Njonjo.

Alieleza kuwa Njonjo alichukia sana mambo ya rushwa na alipenda uwajibikaji katika utendakazi wa wafanyakazi wa serikali.

Bw Wainaina amesema viongozi wa siku hizi ni watu wanaojitakia makuu kwa kujihusisha na rushwa jambo ambalo Njonjo alipinga kila mara alipohudumu katika utawala wa Hayati Jomo Kenyatta na marehemu Daniel Arap Moi.

Sir Njonjo alivyotambulika na wengi atakumbukwa sana kutokana na msimamo wake mwaka wa 1976 wakati alipinga mjadala wa wanasiasa kubadilisha katiba kuwa rais akitoka uongozini makamu au naibu wake airithi nafasi hiyo mara moja.

Wakati huo baadhi ya viongozi katika bunge walitaka mswada huo upitishwe lakini kutokana na msimamo wake mkali, mpango huo ulizimwa kabisa.

Njonjo atakumbukwa kuwa msimamo wake wa kisheria uliokoa mambo mengi nchini.

Mwanasheria huyo pia alikuwa mbunge wa Kikuyu miaka ya 80 baada ya kustaafu wadhifa wa mwanasheria mkuu.

Pia atakumbukwa na mavazi yake kama suti yenye miraba mieupe ambazo zilimtofautisha na watu wengine.

Watu wanaozielewa tabia zake wanadai kuwa alitaka kazi yake kuendeshwa kwa utaratibu wa kipekee bila kuzubaa.

Wakati wa uongozi wake kama mwanasheria, idara yake ilikuwa na uelewano wa karibu na serikali bila mivutano ya kila mara.

Njonjo amefariki akiwa na umri wa miaka 101 na kwa muda mwingi amekuwa akijituliza kwake nyumbani Muthaiga jijini Nairobi.

  • Tags

You can share this post!

Malawi kutegemea idadi kubwa ya wanasoka wa ligi yao ya...

Uongezaji thamani mazao ya kilimo ndio siri ya kuimarisha...

T L