• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 8:55 PM
Lawrence Munga: Pesa kwangu si hoja, hutumia zaidi ya Sh40, 000 kwa siku kununua pombe

Lawrence Munga: Pesa kwangu si hoja, hutumia zaidi ya Sh40, 000 kwa siku kununua pombe

NA MWANGI MUIRURI 

MWANASIASA wa Kaunti ya Murang’a Bw Lawrence Munga amejitokeza kutangaza kwamba ni sonko wa ajabu ambaye hata mvinyo wa Sh40, 000 kwa siku si hoja.

“Mimi si hivi hivi…Nina akaunti za benki si haba. Nina akaunti ya familia, ya biashara, ya ulevi, ya utukutu…Na zote zimejaa hela kama njugu,” akasema.

Alisema yeye hunywa mvinyo aina ya Whisky kwa gharama ya juu na asichukuliwe kienyeji kama asiyejielewa.

Kujigamba huko ambako kumekuwa katika mitandao ya kijamii kumempata akiombwa msaada na hata muungano wa mashoga na wasagaji katika Kaunti ya Murang’a awe mfadhili wao katika kuafikia ajenda yao ya kutambulika na kukubalika.

Akijibu maswali ya Taifa Leo Dijitali, Bw Munga aliyewania wadhifa wa ubunmge Maragua Agosti 9, 2022 lakini akaangukia pua, alisema ushawishi wake pia sio wa kuchezewa.

Uchaguzi huo ambao Dkt William Ruto alishinda urais ulitwaliwa na Bi Mary wa Maua kama mbunge wa Maragua huku akifuatwa kwa umbali na Bw Antony Chege aliyejizolea kura 12, 633 huku huyo Bw Munga akipata kura 2,156 pekee.

“Mimi naweza hata vunja mtu miguu…Naweza fanya mtu atoweke, naweza nikafinya…Mtu akinichukulia ujinga,” akasema Bw Munga ambaye kwa sasa ni mwanachama wa bodi ya usambazaji maji Murang’a Kusini (Muswasco).

Bw Munga alisema kwamba “mimi hucheza gofu na wadosi tajika katika kampuni kubwakubwa na maafisa wa usalama hapa wananitambua na kuniamini na nikiamua hata kuhangaisha wanataaluma nitafanya hivyo”.

Alisema amebarikiwa na Maulana kiasi kwamba hajalishwi na wanaomchukia.

Bw Munga alisema akiamua kutajirisha mtu, si kibarua kwake kwani ni jambo analoweza kutekeleza chini ya sekunde kadha.

Katika hali hiyo, alisema kuwa amekuwa na mradi wa kusaidia vijana wa eneo hilo kutajirika kupitia kuwachanua kuhusu mianya ya uwekezaji.

“Kunao ninasaidiana nao…Nimechukua Sh20, 000 zao na kila wiki nawapa mazao ya kati ya Sh2, 000 na Sh4, 000. Kisha nawapa beli za nguo za mitumba waanze biashara,” akasema.

Hata hivyo, kuna kijana mmoja ambaye ameandikisha ripoti iliyonakiliwa kwa kitabu cha matukio kama 04/31/ 07/2023 kituo cha Polisi cha Igikiro kilichoko katika wadi ya Kamahuha akisema mwanasiasa huyo alimtapeli.

Alielezea kuwa pia alimtishia maisha alipomkabidhi Sh20, 000 miezi saba iliyopita na hadi leo hii hajapata bidhaa za kuchuuza kama alivyoahidiwa.

Hata hivyo, Munga baada ya kufahamishwa kuhusu ripoti hiyo na maafisa wa polisi, alirejesha hela hizo.

 

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

Mwanamume Murang’a aangamiza watoto wake wawili kwa...

Azimio wamtaka Rigathi akae kando ya mazungumzo

T L