• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 6:50 AM
Mwanamume Murang’a aangamiza watoto wake wawili kwa kuwakatakata kama kisasi cha kuachwa na bibi

Mwanamume Murang’a aangamiza watoto wake wawili kwa kuwakatakata kama kisasi cha kuachwa na bibi

NA MWANGI MUIRURI 

MWANAMUME kutoka Kaunti ya Murang’a ameenda mafichoni baada ya kuchinja watoto wake wawili wa kiume, wenye umri wa miaka 7 na miaka 3.

Kisa hicho cha unyama kilifanyika manmo Jumapili, Agosti 6 katika kijiji cha Ndikwe, mshukiwa akitambuliwa kama Evans Kang’ethe na watoto hao wakiwa ni Samuel Irungu na Britton Mwangi.

“Hatujui huyu baba watoto alitekeleza unyama huo saa ngapi. Kile kinajulikana ni kwamba kuna mtu wa familia ambaye alipigia majirani simu akifichua kwamba alikuwa amearifiwa na mshukiwa akimfichulia kuua watoto hao,” akasema Bw Moses Njagi.

Njagi alisema kwamba baada ya ujumbe huo kusambaa katika kijiji hicho, majirani walifika kwa mshukiwa mwendo wa saa mbili jioni na hawakumpata.

“Lakini harufu ya damu ilikuwa kali sana katika nyumba ya mshukiwa iliyokuwa imefungwa. Tuliingia ndani kwa kuvunja mlango na ndipo tukapata watoto hao wawili wakiwa wamechinjwa kama mbuzi…Wakiwa maiti,” akasema Bw Njagi.

Majirani walisema kwamba mshukiwa alikuwa ametengana na bibi yake wiki moja iliyopita.

“Sisi katika kijiji hiki sasa tuna uchungu, tumekerwa sana na kisa hiki na tulianza kumsaka mshukiwa lakini hatukumpata,” akasema Bi Alice Njogu ambaye ni jirani.

Kamanda wa polisi Kaunti ya Murang’a, Bw Mathiu Kainga alisema miili ya watoto hao ilipelekwa hadi hifadhi ya wafu Mjini Murang’a.

“Bado tunamsaka ili atusaidie katika uchunguzi. Tunamchukulia kama mshukiwa mkuu,” akasema.

Baadhi ya wanawake katika kijiji hicho walitoa maoni kwamba bibi akikosana na mumewe, asiwe akiacha watoto wa umri wa chini ya miaka 18 na mume ikiwa ataamua kutengana.

Lakini mshukiwa alisemwa kwamba alikatalia watoto hao akisema ni mbegu zake na hangeziachilia zikarembeshe ndoa ya mwingine au zikanawiri katika familia nyingine.

Msako dhidi ya mshukiwa huyo bado unaendelea.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Wito wa viongozi wa kidini Kisii Rais Ruto na Odinga...

Lawrence Munga: Pesa kwangu si hoja, hutumia zaidi ya Sh40,...

T L