• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Man-U imeisha hakuna timu hapo, Ole Gunnar atoboka!

Man-U imeisha hakuna timu hapo, Ole Gunnar atoboka!

Na CECIL ODONGO

ALIYEKUWA kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amekiri kuwa ubabe wa Man-United sasa umeporomoka kabisa.

Solskjaer, 50, aliyepigwa kalamu Novemba 2021 anasema kudorora kwa timu hiyo uwanjani na pia pandashuka zinazoandama wachezaji kibinafsi, kumeifanya kukosa mvuto kwa wachezaji mahiri ambao ingekuwa rahisi kujiunga nayo.

Alisema hayo siku moja baada ya Man-United kulimwa 4-3 na Bayern Munich kwenye mechi ya ufunguzi ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA), katika uga wa Allianz Arena jijini Munich, Ujerumani, Jumatano usiku.

Sasa kocha Solskjaer – aliyewanoa Red Devils kuanzia 2019 hadi 2021 – anasema kati ya wanasoka mahiri ambao wangeimarisha kikosi hicho lakini wakahiari kwenda kwingine ni kama vile Jude Bellingham, Declan Rice na Harry Kane.

Jagina huyo wa zamani wa Man-United alifichua kuwa alitaka kuwasajili Kane na Bellingham ila uongozi wa klabu ukamwaambia haukuwa na pesa.

Kiungo mshambuliaji Bellingham yuko kambini Real Madrid (La Liga), straika Kane yupo Bayern (Bundesliga) naye kiungo mkabaji Rice anadhibit safu ya kati ya Arsenal (EPL). Mastaa hao wote watatu walihamia klabu hizo msimu huu mpya.

Ni katika uzi uo huo ambapo Solskjaer pia alikiri kwamba lilikuwa kosa kubwa kumrejesha nyota Cristiano Ronaldo ugani Old Trafford Agosti 2021.

Mambo yalienda kombo na mwaka mmoja baadaye Ronaldo akajiunga na Al-Nassr ya Saudia Arabia.

“Ulikuwa uamuzi mbaya hata kama nilihisi lazima tungeuchukua. Alipofunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Newacastle, nilihisi amerejea katika ubora wake ila mambo yakawa vingine,” alisema katika mahojiano na jarida la michezo la Athletic.

Akaongeza: “Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo walikuwa wachezaji chipukizi enzi hizo na tuliwasajili. Sasa mastaa ambao wanawika hata wanahofia kujiunga na United.”

  • Tags

You can share this post!

Mwanamume adai yeye ni yatima anayehitaji kuwa na watoto...

Macho kwa Kipchoge akivizia taji la tano la Berlin Marathon

T L