• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
‘Mathe halisi wa Ngara’ atiwa mbaroni

‘Mathe halisi wa Ngara’ atiwa mbaroni

Na NYABOGA KIAGE

Bi Nancy Indoveria Kazungu, anayejulikana kwa jina maarufu Mathee wa Ngara ambaye na mshukiwa mkuu kwenye biashara ya uuzaji bangi kwenye mji wa Nairobi, amekamatwa.

Mwanamke huyo alikamatwa siku ya Jumatatu Agosti 21, 2023 akiwa katikati mwa jiji la Nairobi na makachero wa Idara ya Upelelezi na Jinai (DCI) ambao wamekuwa wakimsaka kwa muda wa wiki moja.

Wiki moja iliyopita, askari walienda kwenye eneo ambalo inadaiwa amekuwa akiuza bangi hiyo na kupata milioni 13 pamoja na magunia 26 ambayo yalikuwa na misokoto ya bangi.

Kachero mmoja wa DCI aliiambia Taifa Dijitali kuwa mwanamke huyo alikamatwa na kupelekwa katika makao makuu yao yanayopatikana kwenye barabara ya Kiambu.

“Alipokamatwa alipelekwa moja kwa moja hadi makao makuu ya DCI ambapo anaulizwa maswali na makachero kabla ya kupelekwa kortini kesho,” alisema kachero huyo aliyezungumza na Taifa Leo.

Mwanamke huyo alikamatwa masaa machache baada ya kuelekea kortini na kusema kuwa askari walikuwa na mpango wa kumkamata na kumshtaki kwa makosa ambayo hakuwa ameyafanya.

 Taifa Leo imeng’amua kuwa mwanamke huyo atapelekwa kortini kesho siku ya Jumanne na kushtakiwa kwa makosa ya kuuza bangi.

Siku ya Jumanne wiki jana, polisi walienda katika eneo mwanamke huyo anadaiwa amekuwa akifanya biashara yake na kuwakamata watu wanne wakiwemo Bi Teresiah Wanjiru, Bw Eugene Jumba, Bw Hillary Jumbo na Bi Sheila Withers.

Hata hivyo, Bi Wanjiru amezidi kukana kuwa hajawahi kuhusika na biashara hiyo huku akisema kuwa ataishtaki Idara ya Upelelezi ya Jinai kwa kumkamata bila kosa.

Kupitia wakili wake, anayejulikana kama Brian Khisa, pindi tu Bi Wanjiru atakapoachiliwa watahakikisha kuwa polisi nao wamepelekwa kortini kwa kumkamata.

  • Tags

You can share this post!

DONDOO: Mke amchemkia mumewe kwa ‘kumla’ kisura...

Vichapo vyatoa pumzi Man United na Chelsea

T L