• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Mbunge ataka Magoha ahojiwe kuhusu karo

Mbunge ataka Magoha ahojiwe kuhusu karo

Na MAUREEN ONGALA

MBUNGE wa Rabai, Bw William Kamoti amemkosoa Waziri wa Elimu, Prof George Magoha kwa kutaka wanafunzi ambao wana madeni ya karo wafukuzwe shuleni.

Alisema atawasilisha ombi katika bunge la kitaifa la kumtaka Prof Magoha aende kueleza msimamo huo wake.Kulingana naye, wanafunzi wengi hutegemea basari kutoka kwa Hazina ya Kitaifa ya Ustawishaji Maeneobunge (NG-CDF) ambazo hazijapokea fedha kutoka kwa serikali kuu.

“Tutamuuliza waziri Magoha kama anajua kuwa kuna watoto ambao wanategemea msaada ya karo kutoka katika hazina ya NG-CDF na hakuna pesa kutoka wizara ya fedha imeenda mashinani,” akasema.

Akizingumza wakati wa hafla ya kukabidhi basi na maabara katika Shule ya Upili ya Chang’ombe iliyo Wadi ya Mwawesa, Bw Kamoti alisema hiki ni kipindi kigumu kwa kwa wazazi wengi baada ya janga la corona kuathiri uchumi wa nchi.Wakati huo huo, aliwalaumu walimu wakuu katika eneo bunge hilo kwa matokeo mabaya ya mitihani wa kitaifa inayoendelea kushuhudiwa kila mwaka.

“Matokeo ya mitihani ya kitaifa katika shule zetu hairidhishi kwa sababu wanafunzi wetu hawapati muda wa kusoma .Kitu kidogo tu humfanya mwalimu anamrudisha mtoto nyumbani. Watoto wanaopata A katika shule zingine hawakosi masomo,” akasema.

Bw Kamoto aliwataka walimu wakuu kuja na njia mbadala ya kuhakikisha kuwa shule zina kitika cha fedha za kujiendelezea ili kuwakomboa wanafunzi na kuwapa muda mzuri wa kusoma.

  • Tags

You can share this post!

Wahudumu walia kuhusu ada mpya za tuk tuk

Kingi aonya maafisa