• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
MCA ashtakiwa kwa uchochezi wa maandamano

MCA ashtakiwa kwa uchochezi wa maandamano

NA RICHARD MUNGUTI

DIWANI wa Wadi ya Makongeni, Nairobi Peter Imwatok ameshtakiwa kwa kuchochea vurugu wakati wa maandamano ya Azimio.

Bw Imwatok aliyeshtakiwa mbele ya Hakimu Mkuu Lucas Onyina, alikanusha shtaka dhidi yake na kuomba aachiliwe kwa dhamana.

Akiomba Imwatok aachiliwe kwa dhamana, Rais wa Chama cha Wanasheria Nchini (LSK), Eric Theuri na wakili Peter Kaluma waliambia korti kuwa “Polisi walikaidi agizo la Mahakama Kuu la kutomkamata mshtakiwa”.

Walilalamika wakidai kitendo cha kumkamata ni cha kuudhi, wakisema maagizo ya mahakama yataanza kuchukuliwa kama mzaha.

Bw Theuri alisema Jaji Diana Kavedza alikuwa ameamuru polisi wasimtie nguvuni Bw Imwatok lakini wakakaidi agizo hilo na kumkamata.

“Nchi hii imegeuzwa na viongozi wa Kenya Kwanza na polisi kuwa taifa lisiloheshimu sheria,” Theuri alisema.

MCA Imwatok alishtakiwa kwa kosa la kuandaa wakazi wa Nairobi kukaidi amri na kushiriki katika maandamano mnamo Julai 6 na 19, 2023.

Mwanasiasa huyo hata hivyo, alikana kusshawishi wananchi kushiriki katika maandamano.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh100, 000. Kesi hiyo itatajwa Agosti 8, 2023 kwa maagizo zaidi.

  • Tags

You can share this post!

Mwanawe Uhuru apinga serikali kumpokonya silaha

Mahakama yaizima serikali kumpokonya Jomo silaha

T L