• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 7:55 AM
Mihadarati: Magoha aunga wanafunzi wapimwe

Mihadarati: Magoha aunga wanafunzi wapimwe

Na WAANDISHI WETU

WAZIRI wa Elimu Profesa George Magoha amepongeza hatua ya Shule ya Upili ya Maranda Boys ya kuwafanyia wanafunzi wake vipimo vya lazima kubaini iwapo wanatumia mihadarati.

Waziri Magoha alisema hatua hiyo ndiyo mbinu hakika zaidi ya kuzuia wanafunzi kutumia dawa za kulevya wanapokuwa nje ya shule.

Akizungumza katika kongamano la walimu wakuu lililoandaliwa katika hoteli ya Acacia Premier, Kaunti ya Kisumu, waziri Magoha alisema kuwa serikali itawachukulia hatua kali watoto wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu.

“Walimu wakuu wasikubali kuwasajili tena wanafunzi walio na historia ya uhalifu. Wanafunzi wanaojihusisha na ushoga na usagaji watimuliwe katika shule za bweni na kupelekwa katika shule za mchana zilizo karibu na makwao,” alisema Profesa Magoha.

Kwingineko walimu wakuu zaidi ya 26,000 waliokutana Mombasa wanataka kufutiliwa mbalii kwa shule za bweni za sekondari kufuatia kuongezeka kwa visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi.

Miezi michache iliyopita, waziri Magoha alikataa pendekezo hilo baada ya walimu hao kumshinikiza litekelezwe. ,Lakini walimu wakuu wa shule za msingi wanasisitiza kuwa shule za bweni za sekondari zibadilishwe kuwa za kutwa ili kuruhusu wazazi kutekeleza jukumu la kuelekeza watoto wao.

“Aina ya tabia ambayo watoto wameanza kuonyesha katika shule za sekondari inaweza kukomeshwa kwa kuruhusu watoto kuwa na wazazi wao muda mwingi waweze kuwashauri na kuwaelekeza na hii itasaidia walimu,” alisema mwenyekiti wa chama cha walimu wakuu wa shule za msingi Bw Johnson Nzioka.

Bw Magoha alisema mtaala mpya wa masomo (CBC),umebadilisha jinsi watoto wanavyohusiana na wazazi wao.

Alisema haya katika hafla aliyohudhuria ya kuweka msingi wa ujenzi wa madarasa ya CBC katika Shule ya Sekondari ya Obwolo, eneo la Siaya.

  • Tags

You can share this post!

‘Niko tayari kuwa rais wa muhula mmoja’

Obure naye atangaza kugombea ugavana Kisii

T L