• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 10:27 AM
Mirema: Dennis Gachoki aachiliwa huru baada ya kukosekana ushahidi

Mirema: Dennis Gachoki aachiliwa huru baada ya kukosekana ushahidi

NA RICHARD MUNGUTI

MSHUKIWA katika kisa cha mauaji ya mtu aliyeshukiwa na polisi kuwa mhalifu hatari Samuel Mugota, eneo la Mirema kaunti ndogo ya Kasarani mnamo Mei ameachiliwa huru baada ya mahakama kuelezwa hakuna ushahidi wa kumhusisha na uhalifu huo.

Hata hivyo Dennis Karani Gachoki aliyeachiliwa na hakimu mkazi mahakama ya Milimani Bi Carolyne Muthoni Njagi atendelea kuzuiliwa kwa siku 14 kuendelea kuhojiwa kuhusiana na visa vya kuwaibia walevi.

Gachoki anadaiwa kuwanywesha watu dawa na kuwaibia watu.

“Uchunguzi katika kesi hii umekamilishwa na hakuna ushahidi uliopatikana wa kumuhusisha na mauaji ya Samuel Mugota,” alisema Bi Njagi.

Upande wa mashtaka ulieleza korti kuwa hakuna ushahidi uliowasilishwa kuwezesha mkurugenzi wa mashtaka ya umma kumfungulia shtaka la kutekeleza mauaji.

Hata hivyo mahakama ilifahamishwa Gachoki alishtakiwa Jumanne katika mahakama ya Makadara kwa makosa ya kuwekea walevi dawa ya kulevya kwenye pombe kisha wanawaibia.

Gachoki, alifikishwa katika mahakama ya Milimani jana baada ya kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga kwa siku 14.

Gachoki alishtakiwa mbele ya mahakama ya Makadara kwa wizi wa Sh1.2 milioni.

Shtaka lilisema mnamo Juni 24, 2021 katika eneo la Mufu Height lililoko Mirema.

Shtaka lilisema mnamo siku hiyo alimlewesha David Manali Kaikai na kumwibia Sh279,000.

Pesa hizi ziliibwa kutoka kwa Benki ya Equity na Sh122,000 kutoka Co-operative.

Pia alimwibia Kaikai bidhaa nyinginezo ikiwa ni pamoja na simu ya kiunga mbali. Jumla ya vitu alizoibiwa Kaikai ni Sh564,637.

Pia alishtakiwa kumlewesha Martin Nambale Wanjala kabla ya kumwibia Sh490,356.

Bi Njagi alielezwa mahakama ya Makadara iliamuru mshtakiwa azuiliwe kituo cha polisi kwa siku 14 kusaidia polisi kukamilisha uchunguzi.

“Naomba hii mahakama itamatishe kesi ya mauaji dhidi ya Gachoki kwa vile hakuna ushahidi wa kumuhusisha na kisa hicho cha kuuawa kwa Mugota,” hakimu alielezwa.

Mshtakiwa atafikishwa katika mahakama ya Makadara baada ya wiki mbili.

  • Tags

You can share this post!

Chebukati aahirisha uchapishaji wa sajili ya wapigakura...

Kijana ashtakiwa kwa kumtusi baba na kuiba simu ya mama yake

T L