• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Mkenya mashakani Tanzania kwa kuishi nchini humo bila kibali

Mkenya mashakani Tanzania kwa kuishi nchini humo bila kibali

Na HADIJA JUMANNE, Mwananchi Communications Limited

Dar-es-Salaam

Raia wa Kenya anazuiliwa katika rumande baada ya kufikishwa kortini kujibu mashtaka ya kuwepo nchini Tanzania kinyume cha sheria.

Abdulkarim Makiadi, 28, alijipata mashakani mahakamani pale msururu wa maswali ya hakimu ulipobaini kwamba hawezi kutambua mikoa nchini humu, ikiwemo eneo alilosema anatokea.

Alipoulizwa na hakimu kuhusu uraia wake, alisema yeye ni raia wa Musoma.

Musoma si nchi bali ni mojawapo ya mji nchini Tanzania.

Akimsomea shtaka lake, wakili wa Serikali Grace Nyalata alidai kwamba Septemba 16, 2023 katika eneo la Jangwani lililopo Wilaya ya Ubungo, mshtakiwa akiwa raia wa Kenya alipatikana akiishi nchini Tanzania kinyume cha sheria.

Alidaiwa kupatikana akiishi Tanzania bila ya kuwa na kibali wala nyaraka za kumruhusu kufanya hivyo.

Alikana kutenda kosa hilo na ndipo hakimu akaanza kumuuliza maswali kubaini kama anaifahamu nchi vizuri.

Hakimu: Wewe ni raia wa wapi?

Mshtakiwa: Raia wa Musoma.

Hakimu: Mhh Musoma?

Mshtakiwa: Ndio.

Hakimu: Unakaa mkoa gani?

Mshtakiwa: Mkoa wa Musoma.

Hakimu: Kijiji gani?

Mshtakiwa: Siani.

Hakimu: Unakufahamu vizuri Musoma?

Mshtakiwa: Ndio.

Hakimu: Musoma wanakaa kabila gani?

Mshtakiwa: Wapare na Wajaluo

Hakimu: Wewe ni kabila gani?

Mshtakiwa: Mjaluo.

Hakimu: Ukiwa unatoka Dar es Salaam unakwenda Musoma unapita mikoa gani? Hebu nitajie.

Mshtakiwa: Morogoro, Mkoa wa Chalinze, Dodoma, Singida, Shinyanga, Mwanza, unaenda upande wa Tarime halafu Mwanza, Musoma halafu mkoa mwingine wa Tarime.

Hakimu: Tarime? Hebu tuambie ukitoka Tarime unaenda wapi?

Mshtakiwa: Mheshimiwa, hapo nimechanganyikiwa.

Hakimu: Halafu umekoea, ukitoka Dar unaenda mkoa wa Pwani, wewe Pwani hujaitaja.

Mshtakiwa: Niliitaja Chalinze.

Hakimu: Chalinze sio mkoa.

Hakimu: Halafu hakuna mkoa unaitwa Musoma.

  • Tags

You can share this post!

Viatu vya Uhuru sasa vyamfinya Rais William Ruto

Wazee Lamu wataka serikali kuwachunguza wanasiasa wenye...

T L