• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Msanii alisha asema usaliti, vurugu zilimtoa machozi

Msanii alisha asema usaliti, vurugu zilimtoa machozi

Na JOHN KIMWERE 

NI ndoto ya kila msanii kuona anaimarika katika kazi zake na kutambulika kote duniani.

Alice Karwitha Kithinji aachwi nyuma ameibuka kati ya wanawake wanaopania kujizolea umaarufu sio haba hapa nchini pia kufikia viwango vya wasanii watajika duniani. Sura na jina lake pengine siyo geni kwa wapenzi wa tasnia ya filamu hapa nchini  ni miongoni mwa wasanii wanaojivunia kuchota wafuasi wengi tu kupitia vipindi mbali mbali ambavyo vimepata mpenyo kupeperushwa kupitia runinga tofauti.

Kando na uigizaji dada huyu ni mratibu wa sherehe (MC) ambaye kisanaa anafahamika kama MC Alisha. Ni dada aliyeanza kujituma kwenye masuala ya maigizo mwaka 2014 pia anayejivunia kuwa MC kwenye hafla mbali mbali ikiwamo harusi kati ya zingine.

”Bila kujisifia kando na kuwa nilikuwa napenda uigizaji nilivutiwa zaidi wakati nilipotazama filamu iitwayo Sarafina yake Leleti Khumalo mzawa wa Afrika Kusini,” amesema na kuongeza kwamba anajivunia kushiriki filamu nyingi tu ambazo zimepata mpenyo kupeperushwa kupitia runinga tofauti nchini.

Binti huyu aliyezaliwa mwaka 1980 ambaye kajaliwa watoto watatu anapania kukuza kipawa chake zaidi anakolenga kuibuka msanii tajika. Anasema anatamani kujituma kiume katika uigizaji akilenga kutinga upeo wa kimataifa kiwango chake Julia Fiona Roberts mzawa wa Marekani.

Alice Karwitha Kithinji msanii anayetamba katika sekta ya uigizaji kinoma…Picha/JOHN KIMWERE

Pia anasema kuwa huvutiwa nao Kate Winslet (Uingereza ), Angelina Jolie na Whitney Houston wote (Marekani) kati ya wengine. Dada huyu anajivunia kushiriki vipindi kadhaa ikiwamo Gavana Series (KTN), Sunday School Academy (KUTV), Kaiguetie (Weru TV), Mchungaji (NTV),  Loko Loko na Varshita zote (Maisha Magic) kati ya zingine.

Pia anadokeza kuwa upande wa muvi amefaulu kushiriki ‘Tuko macho’ iliyopata nafasi kuonyeshwa kwenye hafla ya Toronto Film Festival ambapo humu nchini ilipeperushwa kupitia NTV.
”Tangia nikiwa mdogo nilidhamiria kuhitimu kuwa mwana habari, mtangazaji kwenye runinga pia wakili lakini mpango wangu haukutimia. Hata hivyo nilikuwa navutiwa na masuala ya maigizo,” akasema.
Hata hivyo ndani ya miaka mitano ijayo analenga kuibuka mwigizaji bomba nchini. Kwa wenzake barani Afrika angependa kujikuta jukwaa moja kikazi nao Leleti Khumalo (Afrika Kusini), Mercy Johnson na Ini Edo wote (Nigeria) kati ya wengine.
Humu nchini huwa anapenda sana siku moja kufanya kazi nao Neomi Ng’ang’a na Kate Kamau ambao hushiriki filamu iitwayo Ma Empress. Anashikilia kuwa kwenye juhudi za kupaisha sekta ya uigizaji nchini mara kwa mara serikali inastahili kuandaa hafla za kutambua wanaofanya vizuri wanaume kwa wanawake.
Pia inapaswa kutenga fedha za kuipiga jeki tasnia ya maigizo ili kutoa nafasi za ajira kwa wasanii chipukizi na wakomavu kama ilivyo nchini Nigeria.
 
CHANGAMOTO
”Hapa nchini wakati mwingine msanii ukawia sana bila kupata ajira ilhali ana mahitaji ya kimaisha,” alisema na kuongeza kuwa kitendo hicho huchangia baadhi yao kusepa na kutema uigizaji.
Akiwa mwanafamilia (Single Mother) anapenda watoto ambapo chini ya kundi lake kwa jina Friends of Charitable Hearts kupitia marafiki huchanga fedha za kulisha familia za mitaani(Street families).
Anasema usaliti na vurugu ziliwahi kusababisha alie machozi hali iliyomfanya aamue achukie kuolewa pia kuwa katika mahusiano ya kimapenzi.
Alice Karwitha Kithinji msanii anayetamba katika sekta ya uigizaji kinoma…Picha/JOHN KIMWERE
  • Tags

You can share this post!

Radol alenga kutinga anga za kimataifa katika uigizaji

Ulinzi starlets: Tuna uwezo kutwaa ligi kuu

T L