• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 6:55 PM
Mudavadi apokonya Mutua wizara ya Mashauri ya Kigeni kwenye mabadiliko ya hivi punde

Mudavadi apokonya Mutua wizara ya Mashauri ya Kigeni kwenye mabadiliko ya hivi punde

Na MWANDISHI WETU

Mmoja wa aliovuna pakubwa katika mabadiliko ya hivi punde ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais William Ruto, ni Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi.

Kulingana na mabadiliko yaliyotangazwa na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei, dakika kadhaa kabla ya saa tatu usiku, Jumatano Oktoba 4, 2023, Bw Mudavadi ameongezewa majukumu kwa kushikilia wizara hiyo iliyo miongoni mwa wizara zilizo na ushawishi mkubwa.

Badiliko moja ambalo huenda lilitarajiwa na baadhi ya Wakenya kutokana na sarakasi na malumbano kwenye mitandao ya kijamii ni lile la Bw Moses Kuria ambaye ameondolewa wizara ya Biashara na Uwekezaji hadi sasa kwenye Wizara ya Utumishi wa Umma na Ufanikishaji wa Miradi ya Serikali.

Katika mabadiliko hayo ambayo pia yameathiri baadhi ya Makatibu wa wizara, aliyekuwa Mbunge Maalum wa Ruiru Isaac Mwaura na mwanahabari wa televisheni aliyegombea kiti cha eneobunge la Matuga katika Kaunti ya Kwale Aisha Chidzuga pia wamepata nyadhifa serikalini. Bw Mwaura ndiye Msemaji mpya wa Serikali huku Bi Chidzuga akiwa naibu wake akishirikiana na mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Gabriel Muthuma.

Wengine ambao wameathiriwa na mabadiliko hayo ni aliyekuwa Waziri wa Maji Alice Wahome ambaye amehamishiwa wizara ya Ardhi, huku Aisha Jumwa aliyekuwa anashikilia wizara ya Utumishi wa Umma akihamishiwa ile ya Jinsia.

Dkt Alfred Mutua wa chama cha Chap Chap aliyepokonywa wizara ya Mashauri ya Kigeni amepelekwa ile ya Utalii huku aliyekuwa anashikilia wizara hiyo, Peninah Malonza akihamishiwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Habari zaidi zaja hivi punde…

  • Tags

You can share this post!

Usiku wa UEFA ambao Man Utd na Arsenal waliona giza

Isaac Mwaura ateuliwa Msemaji wa Serikali

T L