• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Muhsin aombolezwa kama shujaa wa uanahabari, kukuza Kiswahili

Muhsin aombolezwa kama shujaa wa uanahabari, kukuza Kiswahili

Na MARY WANGARI

MWANAHABARI wa miaka mingi, Badi Muhsin, aliyefariki Ijumaa akiwa Mombasa na kuzikwa Jumamosi jijini Nairobi, ametajwa kuwa mzalendo aliyechangia pakubwa ukuaji wa utangazaji nchini.

Rais Uhuru Kenyatta alimtaja Muhsin kama nyota wa televisheni aliyekuwa kielelezo kwa watangazaji wachanga.

Mtangazaji huyo wa lugha ya Kiswahili aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 67.

“Alikuwa mtu wa dhati, mwadilifu na aliyejitolea kwa taaluma na mwajiri wake KBC,” alisema Rais Kenyatta kwenye rambi rambi yake.

Naibu Rais William Ruto alisema Muhsin alikuwa mnyenyekevu: “Tutakosa unyenyekevu wake, umakinifu na ufasaha katika Kiswahili.”

Gavana wa Mombasa Hassan Joho aliomboleza kifo cha Bw Muhsin akimtaja kama hazina ya kitaifa.

Naye Gavana wa Kitui Charity Ngilu alikozaliwa Muhsin alisema kifo kimepokonya kaunti yake shujaa.

Mkurugenzi wa Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI), George Kinoti pia alimwomboleza mtangazaji huyo.

You can share this post!

Munya atetea KTDA kuhusu bonasi ya chini ya majani chai

Wizara yatoa onyo dhidi ya matumizi ya dawa ya kuua chawa