• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 11:37 AM
Nikabidhiwe jeshi langu, Jenerali Muhoozi aambia babake, Rais Museveni

Nikabidhiwe jeshi langu, Jenerali Muhoozi aambia babake, Rais Museveni

NA AFP

KAMPALA, UGANDA>>>

MWANAWE Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba amezua gumzo mitandaoni kwa kudai Jeshi la Uganda ni lake.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter (X), Jenerali Muhoozi alisema jeshi la Uganda ni lake na linapaswa kukabidhiwa kwake.

Huku akinukuu hisia za Kanali Jet Mwebaze kuwa “Wafu pekee ndio wameona mwisho wa vita” Muhoozi alisema kwa kuwa bahati inawapendelea wana wa Mungu, hivyo basi atapendelewa kuwa rais wa Uganda siku moja.

“UPDF bado ni Jeshi Langu. Afande Mzee nataka jeshi langu lirudi! Bahati inawapendelea wana wa Mungu! Nitakuwa Rais wa Uganda siku moja!,” Muhoozi aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Aliendelea kuandika, “Nitakufanyia jina kuu miongoni mwa wakuu duniani… Hili ndilo neno la Bwana wa Majeshi. Nilikuchukua kutoka malishoni na kutoka kuwafuata ng’ombe kuwa Mkuu juu ya watu wangu Uganda. Nimekuwa pamoja nawe popote ulipoenda, na nimewaangamiza adui zako wote katika njia yake,” alijigeuza.

Mwezi uliopita Muhoozi, anayejulikana kama Tweeting General, alisema anataka kuwa rais wa Uganda kwa heshima ya mama yake Janet Museveni.

Katika mfululizo wa ‘milipuko’ ya Twitter kuhusu kuchukua madaraka baada ya babake, ambayo pia iliweka upande wa upinzani kwenye vichwa vya habari, Kainerugaba alisema kuwa akiwa rais wa Uganda ndiyo njia bora ya kumthamini mama yake.

“Njia pekee ninayoweza kumlipa mama yangu mkubwa ni kwa kuwa Rais wa Uganda! Na nitafanya hivyo!” alisema.
Uganda itapiga kura mwaka 2026. Museveni ameiongoza nchi hiyo tangu alipoingia madarakani mwaka 1986.

  • Tags

You can share this post!

SHANGAZI AKUJIBU: Mume wangu amefutwa kazi na haniambii,...

Mshukiwa wa uhalifu anayerejelewa kama ‘mzee wa...

T L