• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 12:09 PM
Ombi la mawakili kwa kaimu Jaji Mkuu

Ombi la mawakili kwa kaimu Jaji Mkuu

Na RICHARD MUNGUTI

MAWAKILI jana walitoa wito kwa Jaji Mkuu mwandamizi Philomena Mwilu abatilishe amri ya kusikizwa kwa kesi kwa njia ya mtandao.

Mawakili waliozugumza na Taifa Leo walieleza kutoridhika kwao na agizo kwamba kesi za dharura zishughulikiwe kwa njia ya kiteknolojia.

Akieleza shida wanazokumbana nazo wakati wa kusikizwa kwa kesi kwa njia ya mtandao ,mawakili Alfred Nyandieka na Eric Achoki walisema , “ utaratibu huu wa kusikiza kesi kwa njia ya kimitandao uko na gharama ya juu sana.”

Mabw Nyandieka , Thomas Maosa na Bw Achoki walisema kuwa iwapo mmoja hana pesa za kutosha kununua muda wa maongezi ya simu mmoja hawezi kutetea mteja wake.

Pia walisema kuwa mmoja anaweza kukaa kortini siku nzima kabla ya kuunganishwa na wateja wao “ikiwa wanazuiliwa gerezani.”

“Kusikizwa kwa kesi nyingi kumesitishwa kwa vile itakuwa vigumu kuwasiliana na mashahidi wakiwa nyumbani ama wakiwa katika vituo vya polisi,” alisema Bw Nyandieka.

Wakili huyo alimsihi Jaji Mwilu aimbue mwongozo mwingine wa idadi fulani ya kesi kuendelea kwa siku moja.

Bw Maosa alisema hakimu anaweza sikiza kesi nne au tano kwa majira.

Alisema kati ya saa tatu asubuhi na saa tano mahakama inaweza sikiza kesi tatu na zile zilizosalia sisikizwe saa nane unusu.

“Mahakama inaweza okoa kesi nyingi zinazoahirishwa kila siku katika hali ya kuthibiti kuenea kwa ugonjwa Covid-19,” alisema Bw Maosa.

Wakili mwingine Evans Ondieki aliunga mkono kufungwa kwa mahakama katika kaunti tano zinazohofiwa kuwa na idadi kubwa ya visa vya Covid-19.

Bw Ondieki alisema maisha yako na thamani kuu na “hayapasi kupotea hivi hivi.”

  • Tags

You can share this post!

Karakara ni matunda ya thamani na rahisi kuyastawisha

Wabunge wa ODM wakosoa ubomoaji wa Njiru