• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 2:32 PM
‘Padri na mrembo wake walijienjoi kwa zaidi ya miaka 6’

‘Padri na mrembo wake walijienjoi kwa zaidi ya miaka 6’

NA MWANGI MUIRURI

MWANAMKE aliyekuwa amekesha katika lojing’i ya Murang’a akiwa na Padri wa Kanisa Katoliki Joseph Kariuki aliyeaga dunia asubuhi ya Julai 8, 2023, amekiri kwamba walikuwa wamependana kwa miaka sita.

“Tulikutana na marehemu miaka sita iliyopita akiwa na umri wa miaka 37 nami nikiwa malkia wa umri wa miaka 26 na kwa muda huo wote, tumekuwa tukila bata katika maeneo mbalimbali ya hapa nchini,” akaandika katika taarifa yake.

Aidha, amekiri kwamba Padri huyo hakuwa na haja ya kuzaa naye mtoto “akihofia kashfa kujitokeza kupitia njama yao ya siri kufichuka”.

Aliongeza kuwa kwa wakati huo wote pamoja hakuwa akimshuku padri huyo kuwa na ugonjwa wa kutishia maisha “labda homa ya kawaida na maumivu tu ambayo yangemalizwa na tembe za kujinunulia kutoka kwa duka lolote la dawa”.

Mrembo huyo wa umri wa miaka 32 aliongeza kwamba Padri alikuwa kipenzi cha wengi “na ndiyo sababu akapewa jina la majazi la Karis”.

Mwanamke huyo ambaye jina twalibana kwa shinikizo za sheria za kitaaluma zinazompa haki ya usiri wake amefichua pia kwamba “kimajukumu alikuwa sawa kama ilivyo kawaida yake lakini mambo yakaenda mrama asubuhi punde tu waliporushana roho”.

Amesema kwamba “alianza kufifia na kuwa na shida ya kupumua…nikamshikilia nikimpa huduma ya kwanza lakini nilipogundua hali ilikuwa inamwendea mrama, nikatoka kusaka usaidizi”.

Maji yalizidi unga na mambo yakaishia kuwa mauti kwa Padri huku polisi wakichukua usukani.

“Lakini asubuhi ya saa mbili kidosho alishuhudia padri akisinzia kama aliyeduwaa na pia kuishiwa na uhai. Alikimbia kuita wasimamizi wa hoteli ambao walikimbia kwa chumba na harakati za kumpeleka Padri hospitalini zikaanza,” ripoti ya polisi yasema.

Wasimamizi wa hoteli hiyo aidha walipiga simu kwa kituo cha polisi cha Samura na ambapo maafisa wawili walitumwa kuwajibikia wito.

“Maafisa waliofika hapo walipata Padri akiwa ameondolewa kwa chumba cha kulala na kuwekwa katika gari lake aina ya Toyota Harrier la rangi nyeusi huku amefunikwa kwa shuka,” afisa mkuu wa polisi wa Gatanga Bw Laurence Njeru akasema.

Maafisa hao wa polisi wakiandamana na wafanyakazi wawili wa hoteli na pia kidosho wa Padri walimpeleka mgonjwa hadi katika hospitali ya Kenol lakini ikabainika alikuwa tayari ameshaaga dunia.

Mwili ulisafirishwa hadi mochari ya Mater iliyoko jijini Nairobi huku polisi wakisema mauti hayo yanachunguzwa kupitia taarifa za mashahidi na pia uchunguzi wa kimaabara.

Bw Njeru alisema kwamba chembechembe za pombe na chakula ambacho wapenzi hao wawili walikula zimechukuliwa kwa uchunguzi zaidi huku pia upasuaji wa mwili ukitarajiwa kufamyika kutoa taswira kamili kuhusu mauti hayo.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Uchungu wa kuona pesa za elimu ng’ambo zikizama

Mshukiwa wa mauaji ya mwanariadha anyimwa tena dhamana

T L