• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Ushuru: Wafanyabiashara wa Eastleigh watishia kuhamia nchi jirani

Ushuru: Wafanyabiashara wa Eastleigh watishia kuhamia nchi jirani

Na COLLINS OMULO

WAFANYABIASHARA katika mtaa wa Eastleigh jijini Nairobi, wanatishia kuhamia nchi jirani kutokana na athari za ushuru wa juu unaotozwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nchi za nje.

Serikali iliongeza ushuru wa vifaa vya kielektroniki, nguo, viatu, vipodozi na kufanya wateja kupungua.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa Eastleigh,Hajj Hassan, alisema mwaka wa 2017 ushuru wa kontena moja uliongezeka na kuwa Sh1.9 milioni kutoka Sh1.7 milioni. Mwaka wa 2022, ushuru huo uliongezeka hadi Sh2.8 milioni kwa kila kontena.

“Mwaka huu pekee serikali imeongeza ushuru mara mbili, Juni 2023 ulipandisha kutoka Sh2.8 milioni hadi Sh3 milioni kwa kontena. Julai 2023, Serikali iliongeza zaidi kutoka Sh3 milioni hadi Sh4.4 milioni kwa kila kontena,” alisema Bw Hassan.

“Sekta ya biashara inategemea bidhaa zinazotoka nchi ya nje kwa uzalishaji. Kutozwa ushuru wa juu, kunaweza kuwavunja moyo wawekezaji wa kigeni jambo ambalo linaweza kulemeza ukuaji wa uchumi,” alisema.

Eastleigh imekuwa ikipokea zaidi ya kontena 1,000 za bidhaa zinazoagizwa kutoka nje kwa mwezi, kwa wakati huu inapokea takriban kontena 300-400 za bidhaa.

  • Tags

You can share this post!

Wanajeshi 2 wa Uganda wahukumiwa kwa kutoroka Al-Shabaab...

Ukivurugikiwa na akili, watoto wako nao pia watavurugika...

T L