• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Wanajeshi 2 wa Uganda wahukumiwa kwa kutoroka Al-Shabaab walipovamia kambi

Wanajeshi 2 wa Uganda wahukumiwa kwa kutoroka Al-Shabaab walipovamia kambi

NA MASHIRIKA

MAHAKAMA moja ya kijeshi nchini Uganda imewapata wanajeshi wawili na hatia ya kuwa waoga, wakati wanajeshi wa taifa hilo waliposhambuliwa na wanamgambo wa Kiislamu nchini Somalia mnamo Mei.

Mameja Zadock Abor na John Oluka walitoroka baada ya wanamgambo wa kundi la Al-Shabab kuanza mashambulizi dhidi yao katika eneo la Bulo Marer, kusini mwa jiji kuu la Somalia, Mogadishu.

Karibu wanajeshi 50 wa Uganda waliuawa kwenye shambulio hilo.

Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya (EU) unataka uchunguzi mkali kuanzishwa kufuatia ripoti za mauaji ya karibu watu 100 nchini Burkina Faso mapema wiki iliyopita.

“Karibu raia 100, wakiwemo watoto na wanawake, wanaaminika kuangamia katika mkasa huo wa kikatili,” akasema mkuu wa sera ya Kigeni katika muungano huo, Joseph Borrell, kwenye taarifa.

Amerika pia imekashifu vikali shambulio hilo.

Hadi sasa, haijabainika kuhusu watu waliohusika kwenye shambulio hilo lililofanyika Jumatatu wiki iliyopita katika kijiji cha Zaongo.

Borrell aliurai utawala wa kijeshi nchini humo kutoa ufafanuzi kamili kuhusu kilichosababisha maafa hayo.

Kufikia jana, utawala huo haukuwa umetoa taarifa yoyote.

Burkina Faso imekuwa ikijaribu kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu, ambapo baadhi yao wamekuwa wakiingia katika taifa hilo kutoka Mali.

Utawala huo umekuwa ukiwalazimisha raia kujiunga na vita dhidi ya makundi hayo ya wanamgambo, yanayodaiwa kudhibiti karibu nusu ya taifa hilo.

Karibu robo ya shule zote nchini humo zimefungwa kutokana na wimbi la mashambulio hatari ambayo yamekuwa yakitekelezwa na makundi hayo.

Mkazi mmoja aliwaambia wanahabari kwamba kijiji cha Zaongo kilikuwa miongoni mwa vijiji vichache vilivyokuwa vimebaki ambavyo havikuwa “vimeshambuliwa na magaidi”.

“Ilidaiwa baadhi ya wanakijiji walikuwa wakishirikiana na wanamgambo,” akaeleza.

Jeshi lilichukua uongozi nchini humo mwaka uliopita, ambapo liliapa kukabiliana na makundi hayo.

Kinaya ni kwamba, mashambulio hayo yameongezeka, licha ya ahadi ya utawala huo kuyakomesha ukiwa enzini.

  • Tags

You can share this post!

Waziri wa Afya asihi wakazi wakuze miti kwa matumizi ya dawa

Ushuru: Wafanyabiashara wa Eastleigh watishia kuhamia nchi...

T L