• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Utafiti wabaini ARVs hutumika kunenepesha kuku, nguruwe

Utafiti wabaini ARVs hutumika kunenepesha kuku, nguruwe

Na ALBETINA MENA, Mwananchi Communication Limited

Kamati ya Bunge kuhusu Virusi vya Ukimwi nchini Uganda imepewa taarifa na mamlaka ya dawa nchini humo kuwa kwa miaka mingi, dawa za kupunguza makali ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) zimekuwa zikilishwa mifugo kwa ajili ya kuinenepesha.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, kamati hiyo imekuwa ikichunguza kuhusu jinsi wanyama nchini humo wanavyopewa dawa za kutibu baadhi ya magonjwa na pia kuwanenepesha.

Mkaguzi Mkuu katika Mamlaka ya Kitaifa ya Dawa Amos Atumanya, aliwaambia wabunge Jumatano Septemba 6, 2023 kwamba uchunguzi ulifanyika baada ya tahadhari kutoka kwa umma mnamo 2014, ambapo iligunduliwa kuwa ARVs zimetolewa kwa nguruwe na kuku, lakini ripoti yake haikutangazwa.

“Kulikuwa na wasiwasi kwamba ikiwa tutaiondoa kwa uwiano, hii itamaanisha nini kwa uchumi ikiwa tutakuwa tunauza chakula nje kama nchi? Kwa hiyo tulikuwa tunajaribu kutafuta njia nyingine ambazo tunaweza kudhibiti hali hiyo,” alisema.

Ripoti yao ilibainisha kwamba ARVs zilitumika zaidi kutibu homa ya nguruwe ya Afrika, ugonjwa unaoathiri wanyama hao ambao kwa sasa hauna tiba.

Pia, ilithibitisha madai kwamba dawa hizo zilikuwa zikitumika kutibu ugonjwa wa Newcastle kwa kuku.

Utafiti wa hivi karibuni uliowasilishwa kwa Kamati ya Bunge wiki iliyopita na Chuo cha Afya cha Makerere uliwanukuu watu wakisema kwamba nguruwe waliolishwa ARVs wanakua haraka na kunenepa lakini walikuwa wakiugua mara kwa mara.

Iliripoti kuwa asilimia 33 ya tishu za kuku na 50 za nyama ya nguruwe zilizojaribiwa kutoka sokoni katika mji mkuu, Kampala, na mji wa kaskazini wa Lira, zilikuwa na mabaki ya ARVs.

  • Tags

You can share this post!

Zizi la Man United laungua nyota mwingine akipatwa na...

Gavana Samboja aliyebwagwa uchaguzini...

T L