• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Waasi wa ODM Nyanza wataka wakazi wamteme Raila

Waasi wa ODM Nyanza wataka wakazi wamteme Raila

Na COLLINS OMULO

WANASIASA walioasi chama cha ODM wamewataka wakazi wa Nyanza kujitenga na upinzani na kumuunga mkono kikamilifu Rais William Ruto.

Viongozi hao walisema eneo hilo liko katika nafasi nzuri ya kufaidika katika Serikali ya Kenya Kwanza tofauti na tawala za awali ambazo zilitenga eneo hilo.

Akizungumza wakati wa kikao na wanahabari jijini Nairobi jana, aliyekuwa mbunge wa Nyatike, Edick Anyanga, alisema Rais Ruto ameonyesha nia njema ya kisiasa kwa kulenga miradi mikubwa na kuteua watu kadhaa kutoka ngome za upinzani.

“Tuliona jinsi ziara ya Rais Ruto Magharibi na Kisii wiki jana ilikuwa na mambo mazuri. Ni wakati muafaka sasa eneo la Nyanza kubadilika ili lihisi kuwa ni sehemu ya serikali bila kujali tulivyopiga kura,” akasema Bw Anyanga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Kudhibiti Nyuklia ya Kenya alisema eneo hilo lazima libadili mkondo kabla ya 2027 kwani hawawezi kushikilia msimamo mmoja kila wakati na kutarajia matokeo tofauti.

Wakati huo huo, viongozi wa kisiasa na wataalamu kutoka Nyanza wakiongozwa na Kennedy Ondiek walipongeza serikali ya Kenya Kwanza kwa kuteua watu kutoka eneo hilo.

  • Tags

You can share this post!

Baba azuiliwa kwa siku 14 uchunguzi wa mauaji ya mwanawe...

Wakazi wa Ugunja walalamikia ongezeko la wizi wa mifugo

T L