• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:22 PM
Wamiliki wa matatu wachangamkia kuondolewa kwa kafyu

Wamiliki wa matatu wachangamkia kuondolewa kwa kafyu

Na CHARLES WASONGA

WAHUDUMU wa matatu wametangaza kuwa watarejelea safari za usiku kuanzia leo Alhamisi baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuondoa kafyu na agizo lake kuanza kutekelezwa mara baada ya hotuba aliyoitoa kwenye sherehe za Mashujaa katika uwanja wa Wang’uru, Kaunti ya Kirinyaga jana Jumatano.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Matatu (MOA) Simon Kimutai alisema baadhi ya wahudumu wa magari hayo watahitaji kwanza kuwajulisha wateja wao kwamba wamerejea safari za usiku.

“Baadhi miongoni mwetu tutaanza safari za usiku Alhamisi. Hii ni kwa sababu tutahitaji kutoa matangazo kwa wateja wetu kwamba tunatoa huduma za usiku,” Bw Kimutai akaambia Taifa Leo kwenye mahojiano katika simu.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema MOA imefurahia hatua ya Rais Kenyatta kuondoa kafyu kwani itawawezesha kufidia hasara ambayo wamekuwa wakipata tangu marufuku ya safari za usiku kuwekwa mnamo Machi 29, 2020.

“Tumefurahi kwa sababu sasa baadhi ya wanachama wetu watarejelea safari za usiku. Ama kwa hakika hatua hii itatupunguzia hasara haswa kufuatia kuongezwa kwa bei ya mafuta,” akasema Bw Kimutai.

You can share this post!

Patson Daka afunga mabao manne na kusaidia Leicester...

Ansu Fati sasa kuchezea Barcelona hadi 2027

T L