• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 1:16 PM
Wahamiaji 43 wafariki mashua ikizama

Wahamiaji 43 wafariki mashua ikizama

Na AFP

TUNIS, Tunisia

WAHAMIAJI 43 walifariki Jumamosi baada ya mashua yao kuzama katika Pwani ya Tunisia, limesema Shirika la Msalaba Mwekundu la Tunisia (TRCS).

Wahamiaji hao walikuwa wakisafiri kutoka bandari ya Zuwara, nchini Libya, wakijaribu kuvuka Ziwa Mediterranean kuelekea barani Ulaya.Mkuu wa shirika hilo, Mongi Slim, alisema watu 84 waliokolewa na Jeshi la Maji la Tunisia.

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la wahamiaji wanaojaribu kuelekea Ulaya kutokana na hali ya joto katika eneo la Kaskazini mwa Afrika.Mashua hiyo ilianza safari yake Jumatatu iliyopita ikiwa imewabeba raia kutoka Misri, Sudan, Eritrea na Bangladesh, kulingana na taarifa iliyotolewa na TRCS.

Inadaiwa mashua ilizama baada ya injini yake kuharibika.Wizaya ya Ulinzi ya Tunisia ilisema wale waliookolewa ni wa kati ya umri wa miaka mitatu na 40.

  • Tags

You can share this post!

Siasa ndizo mwiba kwa Mumias Sugar

Watu 400,000 wanakumbwa na njaa Tigray-UN