• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:01 AM
Waislamu mjini Eldoret wakerwa na kauli ya Papa Francis ya ‘kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja’

Waislamu mjini Eldoret wakerwa na kauli ya Papa Francis ya ‘kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja’

NA FRIDAH OKACHI

BAADHI ya viongozi wa dini ya Kiislamu mjini Eldoret katika Kaunti ya Uasin Gishu wameghadhabishwa na hatua ya kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis kupendekeza ndoa za wapenzi wa jinsia moja kubarikiwa na viongozi wa kidini.

Wakiongozwa na mkurungezi wa baraza la FATWAH, Sheikh Abubakar Bini, viongozi wa dini ya Kiislamu wametoa wito kwa viongozi wa kanisa Katoliki nchini Kenya kujitokeza hadharani na kutoa kauli zao kuhusu tamko la kiongozi wao.

“Hatukutarajia kiongozi kama huyo kutoa msimamo unaoenda kinyume na Biblia na Qur’an. Hakuna mtu anayebagua watu hao wa ushoga na usagaji almaarufu LGBTQ, lakini tunachosema ni kwamba vitendo hivyo, vilikatazwa katika Qur’an na Biblia. Hili ni jambo ambalo limetuhuzunisha. Tunatoa wito kwa maaskofu wa Kiafrika watoe msimamo wao. Wajitokeze na kuongea ikiwa ni kweli au uongo. Ni sawa si sawa? Na wakosowe,” alisema Sheikh Abubakar.

Imam Abulaziz Mohamed, amehakikishia Waislamu kuwa watazidi kufanya maandamano dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Upeo ambayo ilitoa nafasi kusajiliwa kwa makundi ya kutetea mashoga na wasagaji nchini Kenya.

“Huu ni ukiukaji wa amri ya Mwenyezi Mungu aliyoweka kuwa jambo kama hili halifai. Hili tutalipinga kwa sababu jambo kama hili huenda litakapopewa nguvu, watu watafanya mambo hayo kwa wingi na tunaweza tukapata adhabu ya Mwenyezi Mungu,” akaongezea Imam Abulaziz.

Kwa siku za hivi karibuni, jamii ya waislamu imekuwa ikifanya maandamano katika sehemu mbali mbali hapa nchini.

Maandamano sawa na hayo ya Eldoret yamefanyika jijini Nairobi.

  • Tags

You can share this post!

Gachagua ‘aingizwa darasani’ baada ya kusema...

Waislamu na wanaharakati wataka majaji waliotoa uamuzi wa...

T L