• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Wakazi wa Shakahola wataka serikali iwajengee kituo cha polisi

Wakazi wa Shakahola wataka serikali iwajengee kituo cha polisi

NA ALEX KALAMA 

JAMII katika eneo la Shakahola, Kaunti ya Kilifi, inaiomba serikali ya kitaifa kujenga kituo cha polisi ili kuboresha hali ya usalama eneo hilo.

Kulingana na mzee wa kijiji wa eneo hilo Bw Changawa Mangi, huenda maovu zaidi yakafanyika katika msitu wa Shakahola operesheni ya ufukuzi itakapokamilika iwapo hali ya usalama haitaboreshwa.

Mzee Mangi aidha amesisitiza haja ya kituo hicho kujengwa katika shamba la Mackenzie ili kukabiliana kikamilifu na uovu unaoendelea.

“Sisi watu wa Shakahola bado tuna wasiwasi na tunaomba uchunguzi zaidi humo shambani. Mimi kama mzee wa kijiji maoni yangu ni kwamba pawekwe kituo cha polisi hapo msituni polisi wawe wakituchunga Chakama nzima,” amesema Bw Mangi.

Kwa upande wake Joshua Mutinda mfanyibiashara eneo hilo ameeleza kuathirika kwa biashara zao kutokana na changamoto zinazoathiri eneo hilo kwa sasa.

Haya yanajiri huku Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure kindiki akitarajiwa kufanya ziara ya kiusalama katika eneo hilo hapo kesho Jumanne.

“Tulijenga maduka ya nafaka na bidhaa nyingine tukaanza kuuzia watu hawa lakini mwezi wa tatu hali ikageuka ghafla. Kumbe tulivyokuwa tunawaelewa sivyo, tumeathiriwa kibiashara maana hata njahi, mahindi, pojo na maharagwe yameanza kuharibika,” amesema Bw Mutinda.

  • Tags

You can share this post!

Mnifuinge gerezani ni salama kuliko nyumbani –...

Walioshutumu Nyeri kwa kuajiri washika panya…New York...

T L